Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Siku 5 mtuhumiwa wa mauaji mfanyakazi TRA bado kudakwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE 
Siku 5 mtuhumiwa wa mauaji mfanyakazi TRA bado kudakwa
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam linaendelea kumsaka mfanyabiashara na mkazi wa Mbweni Dar es Salaam, Isaya Mzava anayedaiwa kumuua mke wake ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Irene Mzava.

Ni siku ya tano sasa tangu kutokea kwa mauaji hayo na kisha mtuhumiwa huyo kukimbia kusikojulikana. Irene kabla ya umauti kumfika alikuwa akihudumu TRA Tegeta kitengo cha magari, alifikwa na umauti usiku chumbani kwake ambapo alikuwa amelala na mumewe.

Akizungumza na HabariLEO, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai alibainisha kuwa hadi kufikia jana jeshi hilo lilikuwa bado linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo.

Alisema, “tangu kutokea kwa tukio hilo askari wameingia mtaani kumsaka mtuhumiwa huyo namba moja ambaye hadi leo(jana) bado jeshi linazidi kumsaka.”

Siku moja baada ya tukio hilo, mtoto wa Irene, Calvin Isaya alithibitisha kutokea kwa kifo cha mama yake na kueleza kuwa ilikuwa mapema kuzungumzia kifo cha mama yake kwa kuwa suala hilo linashughulikiwa na Polisi.

HabariLEO ilipopita Mbweni nyumbani kwa Irene juzi haikuona shughuli zozote za msiba na geti la nyumba hiyo lilikuwa limefungwa

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments