Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Spika Ndugai:Nimekosa mimi nawomba radhi watanzania

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai amewaomba radhi watanzania wote kwa kutoa kauli ambayo ilizua sintofahamu kuhusiana na mikopo ya serikali na madeni ya nchi.

Spika Ndugai ameomba radhi hiyo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Bunge jijini Dodoma.

“Wengi wameumizwa na kauli yangu, wapo waliopata shida ya kutukanwa na wapo waliosumbuliwa waniondoe kwa sababu ya hao wote mimi nimebeba jukumu la kuomba radhi, Nimekosa mimi, nimekosa sana, Mungu anisamehe, watanzania nisameheni, nawaomba radhi” Spika Ndugai.

Katika kuelezea kauli yake na kuweka sawa juu ya alichokua anataka kuwaeleweaha watu, Spika Ndugai amesema nia yake ilikua kuwasisitiza watu waendelee kulipa kodi na tozo za serikali.


 
“Tarehe 26 kulikua na mkutano wa kinamama wa Mikelile na katika mazungumzo yetu tulikua tunajadili mambo ya maendeleo ya nchi na namna nchi inavyoweza kujikwamua kiuchumi, na nilisisitiza qatu walipe kodi, tozo na malipo yote ya serikali ili kupandisha uchumi wa nchi, nia yangu ilikua hiyo tu hakukua na nia yoyote ya kuokashifu serikali.” Alisema Spika Ndugai.

Spika Ndugai aliendelea kufafanua kuwa baada ya kauli yake ya kuhimiza tozo na kujikwamua kiuchumi yaliibuka maneno mengi ya mitandaoni ambayo yalimuonesha alimkashifu Rais Samia Suluhu Hassan na alishindwa kujibu kwa kuwa alikua anaumwa.

“Sasa wakati yote hayo yanatokea mimi nilikja mgonjwa kitandani, sikuweza kupata nafasi ya kujibu chochote lakini nimeumizwa sana kuonekana namkashifu Mkuu wa nchi,” alisema.


Katika kuuelezea mkopo wa Sh Trilion 1.3 ambao umefanya miradi ya maendeleo nchi nzima, Spika Ndugai amesema jimboni kwake wamepata fedha nyingi ambazo zimekamilisha miradi mingi ya elimu na kupitia mafanikio hayo anaishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kujali wananchi.

“Haijawahi kutokea fedha nyingi zikaelekezwa kwa wananchi kama awamu hii, sisi Kongwa ukiacha hizo za madarasa bado tuliongezewa milioni 470 kwa shule nyingine mbili za vijijini. Nitakua mtu wa kubeba dhambi kama kwa mafanikio hayo sitamuunga mkono Rais wetu.” Aliongeza Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai amesema kuwa haijawahi kutokea utekelezajinwa bajeti ya nchi ukaenda kwa mpangilio kama ilivyopangwa kama mwaka huu wa bajeti wa Rais Samia, huku akisisitiza kuwa kila fedha imeenda sehemu iliyopangwa.

Tarehe 26 mwezi desemba mwaka 2021, akiwa Kongwa Spika Job Ndugai wakati akiongelea umuhimu wa tozo kwa wananchi kiuchumi, alinukuliwa akisema nchi hii ikiendekeza mikopo bula kujitafutia vyanzo vya kipato itauzwa, na baadae Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kusaini mkataba wa SGR, alisema ni lazima Nchi iendelee kukopa ili kuendeleza miradi ya maendeleo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments