Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Steve Nyerere Ashusha Ujumbe Mzito Mtandaoni

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMSANII maarufu wa Filamu nchini Tanzania ambaye anafahamika kwa jina la Steve Nyerere, ameandika ujumbe ambao umeacha mswali mengi yasiyo na majibu miongoni mwa shabiki wake.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram amepakia picha yake ambayo ameiambatanisha na ‘ caption’ isiyo na uwazi kwa shabiki na wadau wanaomfuatilia.

Steve Nyerere amebainisha kwamba kuna wakati inawezekana kama mtu akawa anapitia kipindi ambacho mambo yanayotokea hayaamini kabisa, sababu yanaweza kuwa nje ya malengo aliyojiwekea.

Amefunguka kuwa binafsi inapofika hali hiyo jambo la msingi analolifanya ni kufumba macho kisha anavuta pumzi kwa ajili ya kutuliza akili na kumuomba mwenyezi Mungu.


 
Amebainisha kuwa anamuomba mwenyezi Mungu maana anaamini huenda yote yakawa yanatokea kwa makusudi maalumu, hivyo hamna haja ya kukata tamaa katika maisha yake yote.

Ameongeza kuwa watu wanaweza kumfanyia vitimbwi vya kumchafua kwa wenzake lakini bado kwa mwenyezi Mungu thamani yake inabaki kubwa kuliko kawaida.

Hivyo kama yupo mtu anayepambana kutengeneza mazingira mabovu ajue kwa Mungu huwa hana ubaguzi katika utoaji wa baraka kwa waja wake bali huzingatia muda anaoutaka mwenyewe.

“Wakati huamini yanayotokea kwenye maisha yako, funga tu macho yako na uvute pumzi, na useme, yaa Allah najua huu ni mpango wako nisaidie kupitia hii hali. Na ndio maana ni rahisi sana kumfanya mtu aonekane mbaya mbele za watu lakini ni ngumu sana kumfanya aonekane mbaya mbele ya Mungu,” amesema Steve.

Ujumbe wa Steve Nyerere umepokelewa kwa hisia mseto na shabiki wake ambao kupitia eneo la kutolea ‘ comments’ wapo waliohitaji ufafanuzi zaidi ili waelewe lengo lake, lakini pia wapo ambao wameishia kumuunga mkono kulingana na walivyoutafsiri.

Jambo linalochangia kuibua maswali ni kwamba Steve Nyerere ameandika ujumbe lakini bado haujakaa sawa juu ya kitu gani hasa amelenga kupeleka kwa msomaji wake. Yote kwa yote mwenye uwezo wa kutegua kitendawili alichokiibua kwa shabiki anabaki kuwa yeye mwenyewe.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments