1/26/2022

Taarifa Ambazo si Nzuri kwa Wapenzi wa Muziki, Profesa Jay Amelazwa Muhimbili Hali yake Sio Nzuri...TumuombeeTaarifa ambazo si nzuri kwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya ni kuwa msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, @professorjaytz amelazwa kwenye Hospitali ya Muhimbili huku hali yake ikiwa si nzuri. Kwa mujibu wa mtu wa karibu na msanii huyo ni kuwa Prof Jize licha ya kuwa anapatiwa matibabu lakini hali yake ilikuwa mbaya sana kiasi cha kulazwa ICU, akifanyiwa transfer toka hospitali ya Lugalo hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Pia Ndugu huyo wa Prof amedai bado madaktari hawajatoa taarifa kamili kuwa legend huyo anasumbuliwa na nini zaidi wamekuwa wakiwaambia ndugu hao kuendelea kumuombea msanii huyo.

Hili liwe letu sote, tumuombee Professor Jay arudi kwenye hali yake ya kawaida inshallah🙏

Source: Clouds Fm © Askofu tza

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger