Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Try Again: Simba Itaitikisa Afrika

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURETry Again: Simba Itaitikisa Afrika
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try again’, amesema mipango ya Simba kwa sasa ni kutawala soka la Afrika na kutetea ubingwa.

Try Again alifunguka kuwa timu hiyo kwa sasa ina mwenendo mzuri baada ya mechi chache na mambo yanavyokwenda atakuja kuonekana mrithi sahihi wa Luis Miquissone kutokana na kuimarika kwa wachezaji kadhaa kwenye timu hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Try Again alieleza kuwa wanataka kulishika soka la Afrika na ndiyo maana wamekuwa makini sana kwenye kutafuta wachezaji ambao wataitumikia timu hiyo kwa sasa na dalili za sasa zinaonyesha kuwa wanakwenda kulitimiza hilo.

“Tunakwenda kuliteka soka la Afrika, hiyo ndiyo mipango yetu, timu sasa imeanza kuimarika na kuna wachezaji nyota wameanza kuonyesha kuwa wao ni wa levo nyingine kabisa, tutawaona kina Miquissone wapya muda siyo mrefu.


 
“Tupo makini kwenye kufanya usajili lengo kubwa ni kuwa na timu imara zaidi itakayotikisa kwenye levo za kimataifa,” alisema Try Again.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments