Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Vita imepamba Moto, Burna Boy Amvua Nguo Shatta Wale

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Burna boy hajabaki nyuma, ameamua kumjibu tena Shatta wale kwa kuendelea kuyamwaga hadharani mazito yenye kumuhusu msanii huyo, kwa kusema kipindi alichokuwa karibu na Shatta Wale nchini Ghana aliwahi kushuhudia matukio mengi ya ajabu yaliyokuwa yanafanywa na msanii huyo.


Na kwamba kuna siku alijaribu kutaka kumbaka msichana mmoja ambae jina lake amelihifadhi, na hiyo ndio sababu kubwa ya Burna kutaka kumvujisha Damu na kuyanyofoa meno ya Wale.


Burna amesema kwamba anauhakika kuwa Shatta amewahi kufanya vitendo vya ubakaji kwa wasichana wengi huko nchini Ghana, na pengine hata Mama mtoto wake anaweza kueleza ukweli wote kwa undani zaidi kuhusu suala hilo.

Pia amemshutumu Shatta Wale kuwa muongo, Muhuni, na mshamba, aliyetengeneza habari ya uongo (kiki) ya kwamba amepigwa risasi hali ya kuwa taarifa hizo ni za uongo.


Pamoja na yote aliyoyaorodhesha, Burna Boy ameweka msisitizo kuwa hata magari yote ambayo Shatta Wale anasema anayamiliki, Ukweli ni kuwa ameyakopa, ikiwamo Rolls Royce aliyodai amenunua.


Licha ya kumvua nguo, Burna amesisitiza kuwa yeye ana pesa na mafanikio makubwa kuliko Shatta Wale na kwamba hata akiwachanganya yeye na babu yake bado hawatafikia kiwango cha pesa anazomiliki.


“Shatta  hawezi kunionyesha nyumba, kwa sababu hana.” aliongeza Burna Boy.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments