1/18/2022

Wanandoa Ambao Hawajashiriki Tendo la ndoa Miaka 18 Wakumbukwa na Mungu

 


Wanandoa wawili wanaotokea katika eneo la Murang’a nchini Kenya wamepata kila sababu ya kutabasamu baada ya wasamaria wema kuwazawadia nyumba ya mawe baada ya kuishi na watoto wake katika hali mbaya kwa miaka mingi.


Peter Waweru, ambaye amepooza kwa miaka mingi baada ya kuugua alikuwa akiishi na familia yake kwenye kibanda ambacho kilikuwa karibu kuporomoka, kwa bahati nzuri, wasamaria wema wakiongozwa na mwanamuziki wa nyimbo za Kikuyu, Anne Lawrence, waliguswa na hali mbaya ya familia hiyo na kuanza kampeni mtandaoni ya kumjengea Waweru na familia yake nyumba na vyoo vya hadhi.


Wakati wakisimulia kisa chao kwa watu waliohudhuria hafla hiyo, Anne Lawrence alisema mke wake Waweru, Margaret amesimama na mumewe na hata kuwa mtafuta riziki wa familia hiyo baada ya kuugua kwa mumewe.


“Mwanaume huyu aliugua miaka saba iliyopita, na mkewe amekuwa akisimama naye. Amedhihakiwa sana na watu wa jamii hii,” alisema. Waweru aliugua kifua kikuu na kupooza na hivyo mkewe akachukuwa majukumu. “Aliniambia shujaa wake atakuwa mke wake na ikiwa atazungumza juu ya mtu yeyote mkubwa, mtu huyo atakuwa mke wake,” Anne alisema.

Familia hiyo ilipokea nyumba nzuri pamoja na samani na kulingana na mwanamuziki huyo, Waweru na mkewe hawakuwa wameshiriki tendo la ndoa kwa zaidi ya miaka 18.


Alisema katika hotuba yake. Kwa upande wao wanandoa hao, waliwashukuru watu waliowafaa kwa kuwasaidia kwani walihitaji sana msaada huo. Katika ukurasa wake wa Facebook, Anne hakuweza kuficha furaha yake baada ya kukamilika kwa mradi huo.

“Zaidi ya miaka 18 hawajalala kitandani katika ndoa yao usiku wa leo ni kama fungate kwao. Asante Yehova kwa kututumia,” aliandika mtandaoni.


Mradi huo ulioanza mwishoni mwa mwaka 2021, ulimalizika mnamo Januari na hivi majuzi, wasamari wema, marafiki na familia walikusanyika katika nyumba ya wanandoa hao kwa karamu ya ufunguzi mzuri wa nyumba hiyo yenye vyumba vingi.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger