3/04/2022

Afariki akifanya Tendo la ndoa
Mwanaume mmoja amefariki dunia wakati akiwa faragha na mpenzi wake katika nyumba ya wageni kwenye ghorofa moja jijini Nairobi.

Taarifa za polisi zinasema, Joseph Ngaruiya, 40, anadaiwa kupata shida ya kupumua akiwa na mpenzi wake katika vyumba vya Myra huko Kilimani mnamo Jumatatu, Februari 28, 2022.

Siku ya tukio hilo, Ngaruiya aliingia katika nyumba hiyo iliyoko kando ya Barabara ya Kindaruma kabla ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 25, aliyejulikana kama JM kufika.

Dakika chache baadaye, mpenzi huyo, ambaye inasemekana ni mfanyakazi wa KRA, alitoka nje ya nyumba hiyo ghafla, huku akipiga mayowe, akisema mpenzi wake alikuwa ameanguka na kufariki dunia.


Polisi walitembelea eneo la tukio wakiwa na wahudumu wa afya ambao walithibitisha kuwa alikuwa amefariki na waliupeleka mwili wake katika makafani wakisubiri uchunguzi wa maiti.

Katika ombi lililowasilishwa kortini Jumatano, Machi 2, JM, alipohojiwa, alikiri kwamba waliingia ndani ya nyumba hiyo saa kumi na mbili jioni na walipokuwa wakifanya mapenzi, Joseph alianza kuhema kwa sauti kabla ya kuanguka.

Mwanamke huyo aliwaambia polisi kwamba alijaribu kumuuliza marehemu alikuwa na shida ipi lakini hakumjibu, jambo lililomfanya kutafuta msaada kutoka kwa usimamizi wa jengo hilo na wakati huduma za dharura zilipofika, tayari alikuwa amefariki dunia.


Afisa mpelelezi aliiambia mahakama kuwa timu ya maafisa wa polisi kutoka eneo la Kilimani walitembelea eneo la tukio na kukuta mwili wa Ngaruiya ukiwa umekaa huku ukiegemea ukutani.

Msako ulifanyika katika nyumba hiyo na dawa kadhaa za aina mbalimbali, vileo na vinywaji baridi vinavyoaminika kuwa vya marehemu vilipatikana.

Serikali ilimtaka Hakimu Zainab Abdul kuwapa siku 14 za kufanya uchunguzi wa maiti na kuvifanyia uchunguzi vitu vilivyokutwa ndani ya chumba hicho ili kubaini kilichosababisha kifo chake.

Wapelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai DCI wanataka mpenzi huyo wa marehemu Joseph Ngaruiya, akamatwe na kuhukumiwa

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger