3/16/2022

Afrika Kusini yaidhinisha mpira wa mviringo kwa wanawake kuzuia maambukizi ya HIVAfrika Kusini imeidhinisha matumizi ya mpira wa mviringo mithili ya pete liyoundwa ili kupunguza hatari ya maambukizi ya HIV kwa wanawake.


Ni hatua muhimu katika nchi ambayo karibu theluthi mbili ya maambukizi mapya miongoni mwa wanawake.


Pete hiyo ambayo iliidhinishwa nchini Zimbabwe mwaka jana na bado inaendelea kufanyiwa majaribio katika mataifa kadhaa ya Afrika ina kiwango cha ufanisi cha hadi asilimia 50.


Inafanya kazi kwa kutoa polepole dawa ambayo inapunguza mambukizi ya HIV katika uke na inabadilishwa kila mwezi. Ni mbadala wa dawa zingine zilizopo ikiwa ni pamoja na dawa ya kumeza kila siku.


Mamlaka ya udhibiti wa Afya nchini Afrika Kusini imeidhinisha matumizi ya mpira huo wa mviringo kwa wanawake wenye umri wa miaka 18 na zaidi. Hata hivyo, uzinduzi wake utachelewa kwani idara ya afya inachunguza ufanisi na gharama za pete

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger