Ajali ya Basi na Lori Yaua Watu 22 Morogoro...Rais Samia Atoa Salamu za Pole

Watu 22 wamefariki dunia huku zaidi ya 30 wakijeruhiwa baada ya basi lenye namba za usajili T 732 ATH mali ya Kampuni ya AHMEED linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Tanga kugongana uso kwa uso na lori lenye namba IT 2816 katika eneo la Melea kibaoni barabara ya Iringa-Morogoro.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Muslim amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Malela wilayani Mvomero mkoani Morogoro baada ya basi la kampuni ya Ahmed likitokea Mbeya kwenda Tanga kugongana na Lori la lilikokuwa likisafiri kwenda nje ya nchi.


"Ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Machi 18, 2022 majira ya saa 10 na nusu jioni, eneo la Melea Jibaoni, njia panda ya Kilosa katika barabara kuu ya Morogoro - Iringa wakati Lori hilo likijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki ndiyo likagongana na basi hilo, yakanasana na kusababisha vifo vya watu 13 papo hapo",amesema.


Nimesikitishwa na vifo vya watu 22 vilivyosababishwa na ajali ya basi kugongana na lori katika eneo la Melea Kibaoni, Morogoro. Nawapa pole wafiwa, nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka. Nawasihi watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za barabarani.


______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad