3/06/2022

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Geita vs Yanga"1: POINTI 3 NGUMU NA ZA THAMANI KATIKA BEGI LA WANANCHI👏 Wanarudi Dar Es Salaam miili ikiwa imechoka Lakini mioyo yao itakuwa yenye furaha sana..

2: Kuwakosa 'Key players' wake baadhi, dhidi ya Geita iliyo kwenye 'Form'.. Bila shaka ilihitaji wachezaji wa Yanga kuvuja jasho jingi kuondoka kibabe pale CCM Kirumba

3: Tactically mechi ilikuwa ngumu. Tofauti ya aliyeshinda na aliyeshindwa ni CLASS! Ubora wa wachezaji ndio KEY WORDS! Geita walitengeneza Nafasi nyingi Lakini walikosa 'Class' ya Mayele mbele ya Lango la mpinzani

4: Bao sekunde ya 33 katika Dakika ya kwanza.. Kwenye Football muda ule ni 'concentration Time'.. Ni nyakati ambazo mabao yanafungwa kwa sababu ya wapinzani kuchelewa kuingia mchezoni.. Yanga walianza Game kwa presha ya juu.. ikawashtua Geita, Mayele akawamaliza!

5: WELL DONE viungo wa Geita👏 Waliporudi mchezoni.. waliwapa wakati mgumu sana kina Feisal naSure Boy. Hawakuwapa uhuru kabisa wa kufikiria wakiwa na mpira! Walifika haraka kupokonya mipira na haraka wakausukuma mbele

6: MAYELE.. Achana na Umaliziaji wake, rudi tazama hesabu zake pindi ule mpira umedunda. Alimuibia vyema beki na 'kuturn' haraka na hesabu za wapi anakwenda kuuweka mpira kambani.. What A Player 🙌

7: Heshima kwa Bangala.. Heshima kwa Mwamnyeto🙌 Ziko mechi chache mabeki wa Yanga huwa na nyakati ngumu kiwanjani.. Leo ni moja wapo..! Wamepiga kazi sana. Strong hewani, kasi na Timing nzuri ya kucheza krosi

8: George Mpole.. Ni kama aliipania sana mechi! Sehemu za kupress mpira kirahisi akawa anapiga kwa kung'ata meno.. Ni straika mzuri sana akitunza utulivu wake zaidi kwenye boksi

9: Asante Refa Ramadhan Kayoko.. Umetumalizia ule utata wa Refa wa mkoa wa Timu kuchezesha mechi zake.. Ishu ni WELEDI TU🙌 Asante KAYOKO

10: WELL done DIARRA🙌 Utulivu mkubwa sana Leo. Asante Amos Charles Kadikilo.. Nafikiri Nkane anatakiwa kupandisha zaidi kujiamini kwake na kuwa mchezaji mkubwa katika nyakati ngumu

Nb: Imewauma wao na waliowatuma .. 😃

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger