3/07/2022

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Simba Vs Dodoma Jiji"



1: Ushindi mwingine muhimu kwa Mnyama 🦁 .. Clean Sheet nyingine ya Heshima kwa Beno Kakolanya👏 Haikuwa 'WoW Perfomance' Lakini kwa Simba, kitu cha kwanza ni POINTI 3!

2: Nafikiri miili ya wachezaji wa Simba imeathirika na 'Fatigue'. Nafikiri ndio maana wakachagua kucheza mechi kwa Tempo ya kati ili kutunza nguvu kwa ajili ya mechi ya CAF

3: Mpango wa Masudi Djuma ilikuwa ni kwenye kuubana uwanja katikati. Nafikiri ndio maana akacheza na pacha ya 'Nassoro Rasta' na Hoza mbele ya kiungo wa chini, Mgagula.. Nini walilenga kupata?

4: Pressing ya Hoza na Rasta kwenye 'Mid Block' iliwapa ugumu Nyoni na Muzamir kumuona Chama.. Wakafanikiwa kuikata pasi mpenyezo mbele ya uso wao wa goli

5: Plan B ya Simba ilikuwa kwa Banda na Sakho. Kushambulia kupitia pembeni. 1v1 zilipatikana nyingi sana. Nafikiri ile 'anao anao' ya Sakho na Timing mbovu ya krosi kwa Banda ndio yaliwanyima Simba mabao mengi zaidi kutokea pembeni

6: It's Clear Penalty.. George Wawa alishika ule mpira. Naelewa Dodoma walitengeneza presha kwenye tukio lile ili kutaka kutumia 'advantage' ya Simba kwenye kukosa kujiamini kwenye pigo la Penalti.. Bahati mbaya kwao mpira akauchukua CHAMA🙌

7: TRIPLE C kwenye utulivu mkubwa kama Chatu kwenye windo lake🙌 Dodoma walimsumbua kumpokonya mpira, wakampiga na maneno Lakini akatulia.. Jibu lake ni kuwatuma kuuokota mpira kambani sekunde iliyofata..

8: Yule kiungo wa Chini wa Dodoma.. Jezi namba 24, MGAGULA🙌 Ana kimo kizuri.. Nguvu, kasi, pasi nzuri ya kwanza.. Anapewa utawala wa eneo la kiungo. Akipunguza 'usela' kidogo tu, Lile eneo Dodoma wamepata mtu sahihi sana

9: Hongera kwa Refa Elly Sasi👏 Haiwezi kuwa kwa asilimia 100 Lakini Amefanya kazi yake vizuri. Alitulia mno kwenye maamuzi yake. Changamoto ni yule Line 2! Anafika kwa wakati Lakini anafanya maamuzi kwa presha ya mashabiki

10: Well Done Zimbwe Jr👏 Mechi nzuri pia MKANDALA.. Kazi kubwa kwa Masudi Djuma ni kuwafanya viungo wake wa juu kuwa na madhara kwenye kushambulia.. Sio kupiga pasi nyingu tu zisizokuwa na madhara!

Nb: Timu ya Ubingwa ipo, Tatizo ni Mayele na GSM tu 😃

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger