3/04/2022

Aliyesema alipewa kitita cha bilioni 2.1 na Mpenziwe agundulika ni mhalifu wa kimataifa wa kifedhaMwanafunzi wa kike wa taasisi ya ufundi ya Nairobi aliyekamatwa na pesa nyingi mfukoni mwake Novemba mwaka jana anakabiliwa na hatari ya kupoteza kitita hicho baada ya idara ya mamlaka moja ya serikali kuwasilisha ombi la kumtaka asahau pesa hizo ikizitaja kama zinazotoka katika shughuli za uhalifu.

Katika ombi lililowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Nairobi, Mamlaka ya Kuokoa Mali (ARA) imedai kuwa imemaliza uchunguzi wa akaunti za kifedha za Felesta Nyamathira Njoroge.

Wakili Stephen Githinji, akisema kwa niaba ya mamlaka hiyo alisema Felesta ni mwanachama wa kundi la kimataifa la wahalifu wa kifedha kwa kikombo ‘money-launders’.

“Tumegundua kuwa yeye ni mwanachama wa kundi tata la kimataifa la uhalifu wa kifedha linalohusisha raia wa mataifa mbalimbali likiwemo taifa la Ubelgiji kulikotoka pesa alizopokea kwa kisingizio kuwa ilikuwa zawadi kutoka kwa mpenzi wake,”


 
ARA sasa inataka shilingi bilioni 2.1 za Felista zilizo katika benki ya Co-operative na milioni tano zingine zilizo katika benki ya Stanbic zipokezwa serikali kwa tuhuma za kutumiwa na raia wa kigeni wa Ubelgiji katika shughuli zao za kupata pesa za kihalifu.

Novemba mwaka jana, mamlaka hiyo ilifanikiwa kupata agizo la mahakama la kufunga akaunti za benki za Felista kwa muda wa siku 90 ili kukamilisha uchunguzi katika madai ya uhalifu wa kifedha.

Wakili Githinji aliiambia mahakama kuwa baada ya kukamilisha uchunguzi huo, walikuwa wamebaini kuwa mwanafunzi huyo wa umri wa miaka 21 ni mwanachama wa kundi la kimataifa la uhalifu wa kifedha.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

1 comment:

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger