3/04/2022

Anjella "Mimi Sina Mpango wa Kuhama Konde Gang Nipo Sana Pale"Angelina Samson George maarufu Anjella amesema kwa sasa hana mpango wa kuondoka katika lebo inayomsimamia ya Konde Music Worldwide.

Kauli hiyo inakuja baada ya mieizi miwili kupita, rapa Country Boy kuondoka katika lebo hiyo inayomilikiwa na 'Konde Boy' Harmonize.

“Kwa sasa siwezi kutoka Konde Gang, mimi nilishtuka tu ni kitu gani ambacho kimetokea (baada ya country Boy kuondoka). Unajua kuna sababu zipo lakini mawazo yangu mimi sio kutoka kwa sasa, bado nahitaji kutengeneza,” Anjella aliiambia XXL ya Clouds FM.

Sanjali na hilo, nyota huyo jumamosi hii anatarajia kutumbuiza kwenye tamasha la ‘Afro East Carnival’ ambalo litawakutanisha kwenye steji moja nyota wakubwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika.


HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger