3/04/2022

Breaking News: Mbowe Akutana na Rais Samia Suluhu Hassan Baada ya Kutoka Jela


Rais Samia Suluhu Hassan leo Machi 4, 2022 amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu leo, Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki

Aidha, taarifa imesema kuwa Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taila la Tanzania ni kusimama katika haki


Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger