3/04/2022

Diamond Platnumz Kamkimbia HarmonizeDiamond Platnumz ni supastaa wa muziki nchini Tanzania ambaye alipanga kuachia albam take fupi (EP) leo Machi 4, 2022, lakini ameahirisha na sasa itatoka rasmi Machi 11, 2022.

Kuna tetesi kuwa Diamond amemkimbia Harmonize ambaye wikiendi amedhamiria kuteka jiji na tamasha lake la Afro-East linalofanyika kwa siku mbili katika Uwanja wa Tabata-Shule jijini Dar.

Kwa mujibu wa tetesi hizo, Diamond ameshtuka kuwa EP hiyo inaweza isikimbize kutokana na matukio ya Harmonize na tamasha laek.

Diamond ametoa tangazo la ujio wa EP yake hiyo akidokeza kwamba ataiachia Machi 11, mwaka huu, kinyume na tangazo lake la awali kuwa ingetoka Ijumaa ya Machi 4, mwaka huu.


Diamond ametoa jina la ufupisho wake kuwa FOA ambapo pia amewataka mashabiki wake kung’amua kirefu chake.
Baadhi ya mashabiki wamejaribu kung’amua jina la EP hiyo kwa urefu na ubashiri wa mashabiki wengi ni vichekesho tu kwani kia mtu amejaribu kutoa wake ilmradi herufi hizo tatu zinaonekana.
“Father Of Africa,” mmoja alimtania.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger