Freeman Mbowe Abadili Upepo wa SiasaDar es Salaam. Kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan muda mfupi baada ya kutoka gerezani, kimeibua hisia ya mabadiliko ya upepo wa kisiasa uliokuwepo.

Mbowe na wenzake watatu walitoka gerezani juzi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi katika Mahakama ya Makosa ya Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam.

Kiongozi huyo alitoka katika gereza la Ukonga majira ya mchana na kuelekea gereza la Segerea alikowachukua wenzake watatu na kuelekea nyumbani kwake Mbezi Salasala wakiwa wamevalia fulana nyekundu.

Muda mfupi baadaye, Mbowe alizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake akiwa amevalia koti jeusi na suruali ya kaki na usiku huo huo taarifa kutoka Ikulu ilimwonyesha akiwa amefika na kuzungumza na Rais Samia.

Hali hiyo inaelezwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Paul Loisulie kuwa ni ishara ya dhamira njema ya Rais ya kutaka kushirikiana na wapinzani katika kujenga Taifa.

“Kitendo cha kukutana kwa viongozi hawa, kinatoa ishara kwamba wanahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano ili Tanzania iwe na amani na wamezungumza wenyewe kwamba watashirikiana na nimefurahi neno haki limetawala kwenye mazungumzo yao,” alisema.

Aliongeza kuwa anatarajia kuona ushirikiano baina ya Serikali na Chadema, huku Serikali pia ikitengeneza mazingira bora kwa vyama vya siasa nchini kutekeleza majukumu yao yaliyopo kikatiba.

Mbowe alikaa mahabusu kwa siku 227 wakati kesi dhidi yake na wenzake watatu ikisikilizwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kabla ya kuhitimishwa juzi.

Juzi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwasilisha nia ya kutoendelea na kesi hiyo, jambo ambalo liliamsha shangwe na furaha kwa wafuasi wa Chadema.

Februari 18, Mahakama Kuu iliwakuta washtakiwa hao na kesi ya kujibu baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao na kupanga Machi 4 kuwa siku ya washtakiwa hao kuanza kujitetea.

Hata hivyo, kabla washitakiwa hao hawajafikishwa mahakamani, DPP aliwasilisha nia yake ya kutoendelea na kesi hiyo, hivyo washitakiwa hao wakaachiwa huru wakiwa gerezani.

Mwelekeo mpya Chadema?

Kwa upande mwingine kutoka kwa Mbowe na kubadili upepo wa siasa nchini, kumepokelewa na maswali kadhaa, ikiwamo kama chama hicho kimezaliwa upya kupitia kampeni yake ya Join the Chain.

Lakini pia kutoka kwake kunatazamwa pia na namna chama hicho kikubwa cha upinzani nchini kitakavyoshughulikia suala la wabunge 19 walio kwenye mgogoro na chama hicho. Pia kuna masuala kama mwendelezo wa harakati za kudai Katiba Mpya.

Naibu Katibu mkuu wa Chadema Tanzania Bara, Benson Kigaila alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakitaka kukutana na Rais na walishamwandikia barua kutaka kukutana naye.

“Rais amesema mwenyewe kwenye ile clip kwamba ‘wakati anatoka nikadhani ni muhimu tukutane, nimemwomba tukutane’ na mwenyekiti akasema kwamba ‘ameniomba tukutane nikafurahi kwamba ni muhimu tukutane’, kwa hiyo sasa akikuomba mkutane unakataaje, mtu hukatai wito unakataa neno kama litakuwa baya,” alisema Kigaila.

Alipoulizwa kama wataendelea na ajenda yao ya kudai Katiba mpya, Kigaila alisema hiyo ni ajenda yao ya kudumu na ajenda zao hazibadiliki kutokana na matukio kwa sababu Katiba mpya siyo dai la Chadema, bali ni dai la Watanzania, lilianza jana, lipo leo na litaendelea kesho.

“Ni ajenda pekee, siyo kwa ajili ya Chadema peke yake, ni ajenda kwa ajili ya Watanzania wote kwa sababu ndiyo itatafsiri haki hata za wamachinga wanaofukuzwa, haki za vyombo vya habari, haki za wafanyakazi, haki za wakulima,” alisema kiongozi huyo wa Chadema.

Waliyozungumza Ikulu

Akizungumza baada ya kukutana na Mbowe Ikulu, Rais Samia alisema ameona kuna umuhimu wa kukutana naye kuzungumzia mambo mbalimbali na miongoni mwa hayo walizungumza kuhusu umuhimu wa kuaminiana, kuheshimiana na kutenda haki.

“Ndugu yetu Mbowe leo yuko huru ameachiwa na kutokana na hilo nikaona kuna umuhimu wa kukutana naye leo ili tuzungumze mawili matatu, lakini kubwa tulilozungumza kwamba Tanzania ni yetu wote tunatakiwa kushirikiana.

“Na katika hilo muhimu ni kujenga kuaminiana kwa misingi ya haki na kwamba tunaposimamisha misingi hiyo; kuaminiana, haki na kuheshimiana ndiyo tutapata fursa nzuri ya kuendesha nchi yetu na kuleta maendeleo,” alisema Rais Samia. Kwa upande wake, Mbowe alisema katika mazungumzo yao alimshukuru Rais Samia kwa kujali na kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana ili kuhakikisha kwamba wanaliletea Taifa maendeleo.

“Namshukuru Rais kwamba ameridhia tukutane na nikaona ni jambo la msingi sana kuja kumwona Mheshimiwa Rais baada ya kuwa gerezani kwa kipindi cha takribani miezi minane. Nimemshukuru Rais kwa kuwa concerned (kujali),” alisema Mbowe.

Alisema wamezungumza mambo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu yamekwaza uhusiano mwema kati ya chama tawala kinachoongoza Taifa na chama kikuu cha upinzani nchini.

“Tumekubaliana msingi mkubwa wa kujenga Taifa letu katika maridhiano na umoja unaokubalika, ni kusimama katika misingi ya haki na pale neno haki linapotawala basi amani inakuwa ni automatic (inakuja yenyewe).

“Kwa hiyo tumekubaliana kwamba tunahitaji sana kujenga katika Taifa letu na kila jambo ikiwemo Bunge na taasisi yoyote nyingine ya umma, vyama vya siasa, vyama vya upinzani, chama kinachoongoza, vyote viweze kuihubiri haki,” alisema Mbowe.

Alisisitiza kwamba ili kujenga misingi hiyo kuna umuhimu wa kuaminiana, kwa sababu wamekuwa na urafiki wa mashaka kwa muda mrefu. Alisema wanahitaji kusonga mbele kwa kufanya siasa za kistaarabu, za kiungwana, ili kuisaidia Serikali kufanya majukumu yake na Serikali nayo ihakikishe nao wanafanya majukumu yao vizuri.

“Sisi tumempa Mama hiyo assurance, (uthibitisho) naye amesema atatupa hiyo guarantee kwamba hayo yatafanyika na sisi tuko tayari kumpa ushirikiano na tunaomba ushirikiano kwa Watanzania wote, wampe mama ushirikiano, watupe ushirikiano, tuijenge nchi yetu,” alisema Mbowe.

Hali ilivyokuwa Mahakamani

Juzi wakati wa kuanza kwa kesi, mpaka saa 4:30 asubuhi washitakiwa walikuwa hawajafikishwa mahakamani.

Ilipofika saa 4:55 asubuhi, Mahakama ilianza ambapo wakili wa jopo la utetezi, Peter Kibatala aliieleza Mahakama kuwa yeye na mawakili wenzake walikuwa wameshajiandaa kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea lakini wamepokea taarifa kutoka kwa Ofisa wa Magereza kuwa, mshtakiwa wa nne, Freeman Mbowe ni mgonjwa.

Baada ya kueleza hayo, kiongozi wa jopo la mawakili wa Serikali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando aliieleza Mahakama kuwa, hatajibu hoja ya Wakili Kibatala bali anaombi moja ambalo ni DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Atoka gerezani

Majira ya saa 8 mchana, msafara wa Mbowe ulitoka katika gereza la Ukonga ukiwa na magari mawili, moja likiwa ni Land Cruiser V8 alilopanda yeye na washtakiwa wenzake na lingine ni Pick-Up ya M4C iliyokuwa ikiendeshwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu akiwa na baadhi ya wanafamilia.

Msafara huo uliingia katika gereza la Segerea saa 8:30 alikokuwepo mshtakiwa Halfan Bwire na walikaa humo hadi ilipofika saa 10:40 jioni ambapo walianza kuelekea nyumbani kwa Mbowe maeneo ya Mikocheni.

Walifika Mikocheni saa 11 jioni ambapo watu mbalimbali walikuwepo nyumbani hapo wakimsubiri wakiwemo mawakili waliokuwa wanawakilisha katika kesi hiyo, ndugu, majira pamoja na viongozi mbalimbali wa Chadema.

Hata hivyo baada ya msafara huo kuingia ndani, geti lilifungwa hadi ilipofika saa 1 jioni alipotoka Mbowe akiwa kwenye gari lake jeusi na kusimamia nje ya geti.

Waandishi waliokuwa wamepiga kambi nje nyumbani kwake walimwomba azungumze lolote, alishuka kwenye gari na kuzungumza na wanahabari.

Baada ya hapo aliondoka zake lakini baadaye saa 4 usiku, picha na video zilisambaa mitandaoni zikimwonyesha Mbowe na Rais Samia wakiwa kwenye mazungumzo na baadaye kuzungumzia waliyoyajadili.

Waliyozungumza Ikulu

Akizungumza baada ya kukutana na Mbowe Ikulu, Rais Samia alisema ameona kuna umuhimu wa kukutana naye kuzungumzia mambo mbalimbali na miongoni mwa hayo walizungumza kuhusu umuhimu wa kuaminiana, kuheshimiana na kutenda haki.

“Ndugu yetu Mbowe leo yuko huru ameachiwa na kutokana na hilo nikaona kuna umuhimu wa kukutana naye leo ili tuzungumze mawili matatu, lakini kubwa tulilozungumza kwamba Tanzania ni yetu wote tunatakiwa kushirikiana.

“Na katika hilo muhimu ni kujenga kuaminiana kwa misingi ya haki na kwamba tunaposimamisha misingi hiyo; kuaminiana, haki na kuheshimiana ndiyo tutapata fursa nzuri ya kuendesha nchi yetu na kuleta maendeleo,” alisema Rais Samia.

Kwa upande wake, Mbowe alisema katika mazungumzo yao alimshukuru Rais Samia kwa kujali na kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana ili kuhakikisha kwamba wanaliletea Taifa maendeleo.

“Namshukuru Rais kwamba ameridhia tukutane na nikaona ni jambo la msingi sana kuja kumwona Mheshimiwa Rais baada ya kuwa gerezani kwa kipindi cha takribani miezi minane. Nimemshukuru Rais kwa kuwa concerned (kujali),” alisema Mbowe.

Alisema wamezungumza mambo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu yamekwaza uhusiano mwema kati ya chama tawala kinachoongoza Taifa na chama kikuu cha upinzani nchini.

“Tumekubaliana msingi mkubwa wa kujenga Taifa letu katika maridhiano na umoja unaokubalika, ni kusimama katika misingi ya haki na pale neno haki linapotawala basi amani inakuwa ni automatic (inakuja

“Kwa hiyo tumekubaliana kwamba tunahitaji sana kujenga katika Taifa letu na kila jambo ikiwemo Bunge na taasisi yoyote nyingine ya umma, vyama vya siasa, vyama vya upinzani, chama kinachoongoza, vyote viweze kuihubiri haki,” alisema Mbowe.

Alisisitiza kwamba ili kujenga misingi hiyo kuna umuhimu wa kuaminiana, kwa sababu wamekuwa na urafiki wa mashaka kwa muda mrefu. Alisema wanahitaji kusonga mbele kwa kufanya siasa za kistaarabu, za kiungwana, ili kuisaidia Serikali kufanya majukumu yake na Serikali nayo ihakikishe nao wanafanya majukumu yao vizuri.

“Sisi tumempa Mama hiyo assurance, (uthibitisho) naye amesema atatupa hiyo guarantee kwamba hayo yatafanyika na sisi tuko tayari kumpa ushirikiano na tunaomba ushirikiano kwa Watanzania wote, wampe ushirikiano, watupe ushirikiano, tuijenge nchi yetu,” alisema Mbowe.

Hali ilivyokuwa Mahakamani

Juzi wakati wa kuanza kwa kesi, mpaka saa 4:30 asubuhi washitakiwa walikuwa hawajafikishwa mahakamani.

Ilipofika saa 4:55 asubuhi, Mahakama ilianza ambapo wakili wa jopo la utetezi, Peter Kibatala aliieleza Mahakama kuwa yeye na mawakili wenzake walikuwa wameshajiandaa kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea lakini wamepokea taarifa kutoka kwa Ofisa wa Magereza kuwa, mshtakiwa wa nne, Freeman Mbowe ni mgonjwa.

Baada ya kueleza hayo, kiongozi wa jopo la mawakili wa Serikali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando aliieleza Mahakama kuwa, hatajibu hoja ya Wakili Kibatala bali anaombi moja ambalo ni DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Majira ya saa 8 mchana, msafara wa Mbowe ulitoka katika gereza la Ukonga ukiwa na magari mawili, moja likiwa ni Land Cruiser V8 alilopanda yeye na washtakiwa wenzake na lingine ni Pick-Up ya M4C iliyokuwa ikiendeshwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu akiwa na baadhi ya wanafamilia.

Msafara huo uliingia katika gereza la Segerea saa 8:30 alikokuwepo mshtakiwa Halfan Bwire na walikaa humo hadi ilipofika saa 10:40 jioni ambapo walianza kuelekea nyumbani kwa Mbowe maeneo ya Mikocheni.

Walifika Mikocheni saa 11 jioni ambapo watu mbalimbali walikuwepo nyumbani hapo wakimsubiri.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad