Freeman Mbowe:"Hakuna mazungumzo ya maridhiano bila kuambiana Ukweli"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Chama Kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimesema kuwa hakitashirki mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania, TCD utakaofanyika Machi 30 na 31 mjini Dodoma.

Mkutano huo wa maridhiano ya umoja wa kitaifa unatarajiwa kuhudhuriwa pia na Rais Samia Suluhu na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi.

Hatua hii ya Chadema imetangazwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe ambaye amedai kuwa Chadema haijashirikishwa kwenye masuala yaliyopo kwenye ripoti ya TCD ambayo inaamini imeweka kando kipaumbele muhimu cha suala la katiba mpya.


Mbowe amesema "nimemwambia mheshimiwa Rais process (mchakato) yoyote ya upatanisho lazima itanguliwe na ukweli", alisema Mbowe na kuongeza "tunakwenda kuridhiana tulikosea wapi? Wahanga wakubwa wa maamuzi hayo ni Chadema, sisi ndio watu ambao tumepitia tabu hizo kuliko wote, viko vyama vya siasa vinasema uchaguzi ulikuwa wa haki, sisi tumetengwa na tumetengwa kwa muda mrefu, nimemwambia mheshimiwa rais kwanza ukweli kisha upatanishi'' amesema Mbowe

Mbowe ameongeza pia maazimio ya kituo hicho cha demokrasia yana lengo la kuwaondoa kwenye kipaumbele cha katiba mpya.

''kwenye hoja zinazowasilishwa hatuoni suala la katiba, tunaona kuna mkakati wa kuua suala la Katiba, sasa sisi hatuwezi kushiriki''

Hii ni mara ya kwanza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akizungumza kama Mwenyekiti wa chama hicho mara baada ya kutoka gerezani.

Hapo juzi kamati kuu ya chama hicho ilikaa jijini Dar es salaam na kufikia makubaliano kadhaa ikiwemo kutoshiriki kwenye masuala ya TCD, ambayo ni muungano wa vyama vya siasa vye uwakilishi bungeni, na vyama vingine vinavyoshiriki kama wajumbe washiriki.


Kwa mara ya kwanza mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema, Freeman Mbowe amezungumzia mambo aliyojifunza wakati akiwa gerezani.

Amesema kuwa Pamoja na kazi kubwa inayofanya na polisi nchini Tanzania, lakini kuna uovu mkubwa pia unaofanywa na polisi hao.

Amesema kuwa kuna watu wengi ambao wapo kwenye magereza na mahabusu lakini kwa kukosa msaada wa kisheria wanakaa muda mrefu bila kupata haki.

'Mimi kabla ya kwenda gerezani niliwekwa lupango kwa siku tano, kule ndani kulikua na vijana karibu 40, wamekaa kwa wiki tatu, hawana mwanasheria hawana msaada wowote wa kisheria'' anasema Mbowe.

Amesema pia amesema kuwa mbali na madhila aliyopitia gerezani lakini kuna upande mzuri ambao amejifunza na kuwa hajapoteza muda bure.

''Sikupoteza siku ambazo nilikua gerezani, nimejifunza mengi sana, nimejiimarisha kifikra, kimtazamo na hata moyo wangu umebadilika sana'' ameongeza Mbowe.

Hivi karibuni chama tawala nchini Tanzania CCM, kilitaka jeshi la polisi nchini humo kujitathmini kutokana na mwenendo wa matukio kuhusisha jeshi hilo, Mbowe amesema kuwa chama chake wamekua wakilaumu jeshi la polisi kwa muda mrefu na anashangaa kwanini kiongozi wa jeshi hilo hajajiuzulu.

''Hii ni kauli sisi tumeihubiri miaka na miaka, nashangaa Sirro bado yupo ofisini, chama tawala kinasema jeshi la polisi hili lijitathmini , wewe IGP bado uko ofisini? Inatakiwa siku ya pili yake ujiuzulu''

Mbowe na wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi, ambayo ilisababisha wakaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba, baadae kesi hiyo ilifutwa na mwendesha mashtaka wa serikali ya Tanzania.

Suala la wabunge 19

Mbowe amesema kuwa Spika wa Bunge ameshaandikiwa barua na anajua wabunge 19 wa viti maalumu sio wabunge walioteuliwa na chama hicho.

Amesema Baraza Kuu litakaa mwezi ujao tarehe 25 na kama kuna rufaa zao basi zitaonekana .

"Chadema haijawahi kuteua Kamati Kuu na ninarudia tena leo Chadema haijawahi kuteua wabunge wa viti maalumu" amesema Mbowe

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad