Ticker

6/recent/ticker-posts

Gigy Money Ashauriwa na Sky "Nguvu yako Iko Katika Kuongea Utapiga Sana Hela Ukiamua"

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>Ameandika @skytanzania :

"Nakuelewa sana @gigy_money_og hapa. Uzuri wako ni kuwa tayari unajua nguvu yako iko wapi. Nisisitize kwenye maneno yako mwenyewe, watu wanakupenda ukiongea. Hii ni kwasababu, Mungu amekubariki kuwa ukiongea hata kama lengo lako sio kuchekesha, watu wanajikuta wanafurahi, wanacheka etc. Yaani, wewe ukiongea, watu wanafurahi, that’s called entertainment and it can make you a lot of money!

Katika picha kubwa, watu wanapenda maisha yako. Uko free, ukiwa na hela, ukiwa huna, bado unajiamini na ile confidence yako inaonekana ukiwa unaongea. Huogopi, hufeki na unaishi maisha yako kama unavyotaka wewe.

Unatamani kupata views milioni 1 na kuendelea kwenye YouTube, lakini, amini kwamba, hizo views unaweza kuzipata kirahisi mno kwa wewe kukaa tu sehemu, ukarekodiwa video yenye quality nzuri ukiongea hisia zako; Nini unapenda, nini kimekuumiza, kuwa mama kumekuwa na changamoto gani, kumekubadilishaje, unaamini nini katika mapenzi, boyfriend wako wa sasa ana tofauti gani na aliyepita, unajiskiaje watu wakikichukulia wewe ni mjeuri, stress gani kubwa zaidi kwenye muziki, unapenda kula chakula gani, nini hupendi kula, chakula gani unaweza kukipika zaidi, kipi hukiwezi, kipi kinakukera haraka, Myra amefuata tabia ya nani au anapenda nini etc.. (ya kuongea yapo mengi sana).

Au, fanya vlogs, unapokuwa kwenye photoshoot, make-up, studio sessions, location kwenye video, unapokutana na wasanii wenzako, kwenye shows etc, na ongea kuhusu kinachoendelea at the moment. Sio vitu vigeni hivi, vinafanywa na wengi, inspiration yako kubwa unaweza kuitoa kwa Diana Marua mke wa Bahati (kwa East Africa she is the best kwenye content za aina hiyo.).

Unaanzaje? Tafuta videographer (mchanga, wazoefu watakusumbua), nunua kamera, tripod, lapel microphone, lights na laptop, hivi vyote unaweza kuvipata kwa chini ya Milioni 5. Naamini music video nzuri ina gharimu mara mbili au tatu hiyo, so unaweza kuafford ukijipanga.

Huyu videographer awe responsible katika kushoot, kuedit na kuupload content hii kwenye channel yako ya YouTube. Fanya hivyo, your price won’t be the same again, and then thank me later." sky 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments