Harmonize Afunguka Kuhusu Kumpokonya Country boy Gari "Kuna Wadogo zake Wana Uhitaji Zaidi"


Boss wa record label ya KondeGang na mwanamuziki @harmonize_tz ametoa ufafanuzi juu ya fununu zilizoenea kuwa nyota huyo alimnyang'anya gari Country Wizzy punde baada ya kumalizika kwa makubaliano yao ya kikazi.

Kupitia kipindi cha XXL Harmonize ameeleza kuwa miongoni mwa sababu zilizo mfanya rapper @countrywizzy_tz kurudisha gari baada ya kutoka kwenye lebo hio ni pamoja na rapper huyo kutambua uhitaji wa vijana wengine waliopo ndani ya KondeGang.

“Kuhusu kurudisha gari tulikuwa na makubaliano ya pande zote mbili, kama ambavyo nimesema sisi sote ni vijana wenye malengo ya kufika mbali.

“Hata yeye alirudisha kwa kuelewa Konde Gang ni kampuni, kuna wadogo zake hapa ambao wanaweza kuwa na uhitaji zaidi yake yeye! Ndio maana baada tu ya kurudisha haikupita hata week akanunua gari yake mpya,"🎤 #Harmonize

Mbali na hilo Harmonize ameeleza kuwa kuhusu Country kuondoka na na kutomlipisha pesa, lengo halikuwa yeye kupata kitu, bali lengo lilikuwa ni wao kutimiza ndoto zetu kama vijana.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad