Hushpuppi Atapeli Million 926 Akiwa Jela

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Ramon Abbas maarufu kama Hushpuppi amefunguliwa mashtaka mengine mapya ya utakatishaji fedha baada ya kufanya utapeli wa $400,000 sawa na Tsh million 926 akiwa gerezani Marekani.
Waendesha mashtaka wa Marekani waliwasilisha hati mbele ya Mahakama ya Wilaya ya California, Marekani siku ya jana Machi 16, pamoja na ushahidi kuhusiana na Hushpuppi kutenda uhalifu katika ofisi ya magereza.

Hushpuppi anadaiwa kununua kadi za benki 58 za wizi mtandaoni ambazo hutolewaga maalum kwa ajili ya malipo kwa raia wa Marekani waliopata athari za kiuchumi kutokana na majanga kusaidiana na mtu aliyejiita AJ aliyekuwa anawasiliana naye na ndiye aliyefanya malipo ya kadi hizo. Hushpuppi alifanya harakati hizo kipindi ambacho wafungwa wanapewa nafasi ya kupiga simu, kutumia computer na mitandao ya kijamii.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad