Ticker

6/recent/ticker-posts

Ismail Aden Rage Aionya Simba Kwa Yanga "Sio Rahisi Kama Mnavyofikiria Kuchukua Ubingwa"

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ameitaka timu hiyo kufanya kazi ya ziada kama kweli wanataka kuishusha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Rage alifunguka kuwa, Simba wapo kwenye nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ila haitakuwa rahisi kwa sababu Yanga ya msimu huu ipo imara zaidi ya misimu mingine ya nyuma.


Akizungumza na Spoti Xtra Rage aliweka wazi kuwa: “Naomba niwe muwazi juu ya suala hili, Yanga wapo imara sana msimu huu. Hivyo Simba wanatakiwa kuwa makini nao sana na wanatakiwa kufanya kazi kweli.

“Ubingwa unaweza kupatikana lakini siyo rahisi kama ambavyo ilikuwa misimu iliyopita, hilo wanatakiwa walijue, wana kazi kubwa ya kufanya.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments