Kimeumana..Rais Putin Aishutumu Ukraine Kutumia Raia Kama Ngao ya Kujilinda..Imegoma Kuwaruhusu Kuondoka


Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Ukraine inawatumia Raia kama ngao ya kujilinda na kusema Ukraine imeomba Safe Corridor ili zitumike kuwaokoa Watu kutoka Ukraine lakini wala haziwaondoi Watu hao "Jeshi letu liliacha kushambulia ili Raia wasio na hatia waondoke kwanza lakini Ukraine imegoma kuwaruhusu Raia kuondoka"

Putin amezifananisha tabia anazodai zinafanywa na Ukraine za kuwatumia Raia kama ngao ya kukwepa mashambulizi na Watu walioamini itakadi za kinazi za Adolf Hitler ambao anasema walijificha nyuma ya Raia kutafuta huruma na kuwatumia kama ngao ya kukwepa kushambuliwa badala kuwaruhusu Raia hao waondoke salama ili mapambano yaendelee.

Kauli ya Putin inakuja baada ya Naibu Meya wa Mji wa Mariupol nchini Ukraine kusema bado Wanajeshi wa Urusi wanaendelea kushambulia Mji huo licha ya makubaliano yaliyofikiwa na Urusi na Ukraine kwamba wasitishe mapigano kwa muda mfupi katika Miji miwili ya Mariupol na Volnovakha iliyokumbwa na mapigano ili kuwaruhusu Raia kuondoka.

Miongoni mwa waliotengenezewa Corridor ili pamoja na Raia wa Tanzania ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Moscow nchini Urusi umetoa taarifa kwa Wanafunzi wote wa Kitanzania walioko kwenye Chuo cha Taifa cha Sumy nchini Ukraine kwamba Serikali ya Urusi imetengeneza Safe Corridor ya Wanafunzi hao kutoka Ukraine kupitia Urusi kuanzia leo March 05,2022 .
#MillardAyoUPDATES
(📹 Ruptly)
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad