Korea Kaskazini Hawapoi Kwa Vitisho Yafanya Jaribio Lake la Tisa la Kombora

 


Korea Kaskazini leo imefanya jaribio lake la tisa la kombora mwaka huu kwa kurusha kombora linaloshukiwa kuwa la masafa marefu kuelekea katika Bahari ya Mashariki mwa Rasi ya Korea siku chache kabla ya uchaguzi wa rais nchini Korea Kusini.

Jaribio hilo limeibua shtuma kutoka kwa serikali nchini Marekani, Korea Kusini na Japan zinazohofia kwamba Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio kubwa la silaha katika miezi inayokuja. 


Baada ya jaribio hilo la hivi karibuni, Waziri wa Ulinzi wa Japan Nobuo Kishi amesema kuwa kasi kubwa ya teknolojia inayoendelezwa na Korea Kaskazini ya kurusha makombora, sio kitu kinachopaswa kupuuzwa na nchi hiyo na maeneo ya karibu.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad