3/07/2022

Lulu Diva Anataka Ndoa, Mtoto

BAADA ya kumpoteza mama yake mzazi miezi michache iliyopita, mrembo kutoka kiwanda cha Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka kuwa, anaomba Mungu ampe mume au mtoto kwa sasa kwa sababu anaona muda wa kufanya hivyo umefika.

 

Diva alisema, kifo cha mama yake kimempa funzo la kuwa, kwa mwanadamu yeyote anahitaji kuwa na familia kwani kwenye maisha lolote linaweza kutokea na mtu ambaye atakuwa msaada ni familia yako.

 

Diva alikiambia Kilinge kuwa, alikuwa msaada mkubwa kwenye kupigania uhai wa mama yake wakati anaumwa na kama mama yake asingemzaa, pengine angekufa kifo cha mateso zaidi kwa kukosa mtu wa karibu zaidi.

 

“Natamani kupata watoto kwa sasa, kwa sababu nimeona umuhimu wa kuwa na watoto kwa kile ambacho kimemtokea mama yangu. Nami natakiwa kuwa na mtoto ambaye atakuja kunizika.

 

“Ndoa na mtoto ndiyo vitu ambavyo nahitaji kwa sasa kwa sababu pia muda na umri wa kuwa na hivyo vitu umefika. Huu ndiyo umri sahihi kwangu kuwa na familia,” alisema.

STORI ISSA LIPONDA

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger