3/04/2022

Mama Kanumba "Nisaidieni Udhamini Nifanye Movie ya Kanumba"

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPAMAMA wa aliyekuwa staa mkubwa wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa anasema kuwa, hakuna kitu ambacho anakitamani kama kutengeneza makala maalum ya Kanumba tangu utotoni hadi kifo chake.


Anasema kuwa, akifanikiwa ataona kuwa kuna kitu kikubwa amekifanya kwa mtoto wake, lakini ukweli ni kwamba hajui ataanzia wapi kwa sababu hana pesa hivyo anaomba udhamini kwa ajili ya kazi hiyo.


Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Mama Kanumba anawaomba wadhamini mbalimbali ambao wanaweza kumuwezesha kwa namna moja au nyingine kuweza kufanya makala hiyo ya mtoto wake kwa sababu itabaki kuwa ni kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavyo.


“Kuna kitu kikubwa ninakitamani sana na hakika roho yangu itatulia sana kama nitaweza kufanya makala ya mwanangu hivyo nawaomba wadau mbalimbali kama wapo waje wanisaidie au tushirikiane kwa jambo hilo, hakika nitakuwa nimeiponya nafsi yangu kwa mawazo,” anasema mama huyo ambapo bado mwezi mmoja Kanumba atumize miaka kumi tangu atangulie mbele ya haki.


Kanumba alifariki dunia siku ile ya Aprili 7, 2012 akiwa ndiye kinara wa Bongo Movies.

Stori; Imelda Mtema, Dar
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger