Mbowe Asema Amewasamehe Wote

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amefunguka na kusema amewasamehe wote waliomfanyia mabaya.

Mbowe alisema hayo jana zikiwazimepita takriban wiki mbili tangu Mahakama Kuu ya Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ilipomwachia huru baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kudai hana nia ya kuendelea na kesi iliyokuwa ikimkabili kwa tuhuma za ugaidi.

Alisema ametoka gerezani akiwa na roho nyeupe na hana kinyongo na mtu yeyote, huku akiwataka wanachama wa CHADEMA nchini nao kutokuwa na visasi bali waendelee kufanya siasa.

Kiongozi hiyo alitoa kauli hiyo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana hivi karibuni.

“Nimesema na ninasema tena, ninatangaza msamaha kwa yeyote aliyefiriki amenifanyia baya. Sina chuki wala kisasi. Nawaomba wana-CHADEMA wenzangu tusiwe na chuki na mtu yeyote katika mapambano haya.


“Mapambana haya ni kupigania ustawi wa watu. Hatuwezi kuutafuta ustawi wa watu wakati tukiwa na kisasi. Kisasi si utamaduni wa CHADEMA wala wa Mbowe. Nimetoka na roho nyeupe kabisa nikiwa tayari kuendeleza mapambano ya kisiasa” alisema.

ALICHOTETA NA RAIS

Pamoja na mambo mengine, Mbowe alieleza kile alichozingumza na Rais Samia Suluhu Hassan muda mfupi baada ya mahakama kumwachia huru.

Alisema alifanya mazungumzo mambo mengi na Rais Samia ikiwamo kujadili njia bora ya kutafuta amani na suluhisho katika kufanya siasa.


“Jambo la kwanza tulikubaliana tuache kuzungumzia neno amani, amani, amani. Tulikubaliana tuzungumzie neno haki. Jambo la pili, nilimweleza kwamba CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani nchini, hivyo maridhiano yoyote yanayofanywa ndani ya taifa hayawezi kufanyika pasipo kukishirikisha CHADEMA,” alisema.

“CHADEMA kipo kuanzia ngazi ya kata, kitongoji, kijiji hadi mtaa, hivyo kukitoa ni jambo ambalo haliwezekani. Jambo la tatu tulizungumza na kukubaliana ni kwamba kila upande ujenge imani kwa mwenzake, tusiishi kwa hofu,” aliongeza.

SAKATA LA MDEE

Kuhusu wabunge 19 wa viti maalumu walioKo bungeni, wakiongozwa na Halima Mdee wanaodaiwa kuwa ni wa CHADEMA, Mbowe alisema chama hakijawahi haijawahi kuteua wabunge wowote.

Alisema Spika wa Bunge aliandikiwa barua na anajua wabunge hao si halali kwa kuwa hawakuteuliwa na chama hicho.


Mbowe alisema Baraza Kuu la CHADEMA litakaa Aprili 25, mwaka huu, na kama kutakuwa na rufani yoyote kuhusu wabunge hao, itashughulikiwa.

KATIBA MPYA

Kuhusu Katiba Mpya, Mbowe alisema mchakato huo ni endelevu, kudumu na hauna kikomo.

Alisema kwa sasa CHADEMA imeamua kujikita kwenye mazungumzo ya kudai katiba mpya na kwamba endapo itashindikana, itatafutwa njia nyingine.

Kadhalika, Mbowe alisema CHADEMA hakitashiriki mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) pamoja na kongamano linalotarajiwa kufanyika Machi 30 mwaka huu jijini Dodoma.


“Machi 21 nimeambiwa kuna kikao cha TCD, CHADEMA tulikubaliana hatutashiriki kwa kuwa hatuna wabunge hadi hali hii itakapobadililllka,” alisema Mbowe.

Kuhusu kongamano la TCD linalotarajiwa kufanyika Machi 30 na 31, mwaka huu, kwa lengo la kutafuta maridhiano ya kisiasa, Mbowe alisema pia CHADEMA haitashiriki
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad