Mbowe ataja mambo matatu aliyozungumza na Rais Samia 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametaja mambo matatu waliyozungumza na Rais Samia Suluhu Hassan walipokutana Machi 4, 2022 baada ya kutoka gerezani, ikiwamo kujadili njia bora ya kutafuta amani na suluhisho katika kufanya siasa.

Mbowe ameyasema hayo leo Machi 18 jijini Dar es Salaama alipokuwa akitoa taarifa ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Machi 16 jijini hapa.

Amesema; “Tulikubaliana aache kuzungumzia neno amani azungumze neno haki. Jambo la tatu nilimfahamisha yeye apende au mtu mwingine Chadema ni Chama Kikuu cha Upinzani huwezi kukiacha nje.”

Akisisitiza kuhusu hoja hiyo, amesema chama hicho kipo kila mahali na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vingine haviwezi kuinyamazisha.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad