Mbowe, Kinana, Lipumba kujadili mkwamo katiba mpya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KITUO cha Demokrasia Tanzania (TCD), kimemuita Mwenyekiti wa Chama cha Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana wajadili sababu za mkwamo wa mchakato wa upatikanaji katiba mpya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa jana Jumanne, na Mwenyekiti wa TCD, Zitto Kabwe akizungumza katika majadala wa nini kianze kupatikana kati ya tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, uliofanyika mtandaoni na kuongozwa na Mwanaharakati Maria Sarungi.

Zitto amesema, vigogo hao wa siasa Tanzania, watatoa maoni yao hayo kwenye mkutano wa TCD, unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Machi 2022, jijini Dodoma, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi.



Amesema, Mbowe na wenzake, wameitwa kujadili sababu za mkwamo huo, kwa kuwa walishiriki kwenye mchakato wa upatikanaji katiba mpya, uliofanyika 2014, ambao walihusishwa katika kupendekeza muda maalumu wa mchakato huo kukamilika.

“Kwenye mkutano tunaoufanya Dodoma mwishoni mwa mwezi wa TCD, kuna ajenda itakayozungumzwa kwa nusu siku, kuhusu minimum reforms, ambao tumewiata ni watu waliouwepo kwenye makubaliano ya 2014, Kinana, Mbowe na Lipumba,” amesema Zitto na kuongeza”

Waje watuambie tulikwamaa wapi na nini kifanyike kukwamua mchakato wa katiba. Kwa hiyo mchakati wa katiba lazima uwepo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad