Mbowe: Sikutaka kesi ifutwe ili dunia ijue ukweli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





MWENYEKITI wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia, Freeman Mbowe amesema licha ya kuwa ugaidi ni kosa linaloweza kumfungisha mtu maisha lakini alimuomba Mungu asifutiwe mashtaka ili dunia ijue ukweli kuhusu jambo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Mbowe ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Machi mwaka huu wakati akizungumza na waumini aliposhiriki ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Azania Front jijini Dar es Salaam.

Tarehe 4 Machi mwaka huu, Mbowe na wenzake watatu alifutiwa mashtaka mbalimbali ikiwemo ya kupanga njama na kufanya vitendo vya kigaidi.

Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali aliwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi iliyokuwa ikiunguruma katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.


 
Pamoja na mambo mengine, akizungumza katika ibada hiyo, Mbowe amesema alishtakiwa kwa kosa zito ambalo wengine wanaona tu ni ugaidi, lakini hawajui tafsiri ya neno ugaidi.

“Shtaka lolote la ugaidi lina kifungo cha miaka 15 kwa uchache hadi miaka 30 na hakuna fanini. Kwa hiyo ni kosa linaloweza kukufunga maisha.

“Lakini nilimuomba sana Mungu anisaidie dunia ijue ukweli kuhusu jambo hili, natambua wako wengi ambao ni ndugu, marafiki ambao walishtuka labda Mwenyekiti Mbowe amefanya jambo fulani ambalo hatulijui,” amesema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad