Mke Amjeruhi Mumewe kwa Mapanga, Kisha Ajinyonga Kuhofia Kupata Kesi ya Mauaji
Mkazi wa kitongoji Kijiji cha Sibwesa wilayani Tanganyika, Mande Emanuel (30) amejinyonga baada ya kumjeruhi mumewe, Dotto Enos (35) kwa kumkata mapanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na shughuli za kilimo.

“Ilitokea sintofahamu ikapelekea ugomvi kutokea ndipo mwanamke huyo aliamua kumpiga mapanga mume wake na kumjeruhi vibaya,”

“Alipogundua mume wake anaweza kufa akahofia kupata kesi ya mauaji, alizunguka nyuma ya nyumba yao akapasua kitenge chake akajinyonga, mume alipelekewa hosptali ya rufaa mkoa kutibiwa,” amesema Kamanda Makame


Katika hatua nyingine Kamanda Makame amesema katika kijiji cha Kapanga wilayani Tanganyika alikamatwa Julias Lyamkolo {63) akiwa na bangi gramu 250.

Inadaiwa kuwa wakati anahojiwa mtuhumiwa huyo alikiri kuwa yeye ni mkulima wa bangi na aliwapeleka polisi kuwaonyesha shamba lenye ukubwa wa ekari 4 alilopanda mahindi na bangi.

“Mtuhumiwa tumemshikilia tunaendelea kumhoji ili atutajie masoko yake na washiriki wake wote tuweze kuwakamata wafikishwe kwenye sheria na bangi tumezifyeka na kuzichoma moto,”
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad