3/20/2022

Morrison, Bwalya wapewa kazi maalum, wawili njeSIMBA wametua salama mjini Cotonou, Benin kwa mchezo wao Kombe la Shirikisho Afrika leo dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, huku Bernard Morrison na Rally Bwalya wakipewa kazi maalumu kikosini kuhakikisha kazi inamalizika mapema.

Viungo hao washambuliaji watapiga mipira yote ya friikiki na kona, huku mabeki wa timu hiyo be wakipewa mapema mbinu za kuepuka kuruhusu mabao yanayotokana na mipira iliyokufa katika mechi hiyo. Simba jana jioni ilipiga tizi la maana kujiweka sawa kwa mchezo huo, huku Asec wakipata mchecheto kila wakikumbuka kipigo cha mabao 3-1 Dar. Kocha Pablo tangu akiwa jijini Dar es Salaam aliwaandaa wachezaji wake kutumia vizuri mipira ya friikiki, huku akiwapa kazi hizo Morrison na Bwalya na kuwakazania mabeki wake katika kujilinda dhidi ya mipira ya krosi na ile ya friikiki inayoonekana kuisumbua timu hiyo kwa misimu minne mfululizo sasa.

Katika mechi dhidi ya Berkane, Simba ilifungwa mabao mawili na Wamorocco ugenini kwa mipira ya friikiki na kona, kisha kutupiwa jingine ikiwa nyumbani dhidi ya timu hiyo, lakini waliotea.

Hata hivyo, katika mazoezi ya mwisho ya jijini Dar Kocha Pablo Franco alikomalia jambo hilo kwa mabeki wake. Pablo alikuwa mkali kwa Kennedy Juma, Pascal Wawa, Erasto Nyoni na Henock Inonga ambao kazi yao ilikuwa kuruka na kuokoa kwa vichwa krosi zilizopigwa na Mohammed Hussein na Shomary Kapombe.


 
Mabeki hao wa kati wallitakiwa kuruka na kuokoa mipira hiyo kwa vichwa vyenye nguvu ili mpira uende mbali na lango lilipo.

Kuna muda walifanya wenyewe ila muda mwingine waliwekewa washambuliaji, Chriss Mugalu, Meddie Kagere na Kibu Denis waliokuwa wanashindana nao.

BM3 NA BWALYA

Pia aliwatumia Morrison na Bwalya kupiga mipira mingi ya friikiki na kona, sambamba na kuwahimiza wachezaji wote kuhakikisha wanatumia nafasi zinazotengenezwa kufunga mabao.


Katika Ligi Kuu Bara tangu kurejea kwa Clatous Chama, Simba imekuwa ikimtumia Mzambia huyo ambaye hajafuatana na timu kwa vile hawezi kuitumika kwa kubanwa na kanuni za michuano hiyo, kwani alishaichezea Berkane.

Kwa namna kocha alivyokuwa akiwakazania wachezaji hao, maana yake kama BM3 na Bwalya wataanza wote kikosini watapeana zamu kupiga mipira yote iliyokufa, lakini kama mmoja atakuwa nje, aliyepo uwanjani atalibeba jukumu hilo kabla ya kuja kupokewa na wenzake.

Mara baada ya timu kutua Cotonou na kujichimbia kwenye hoteli ya Azalai, walikuwa bize kufanya vipimo vya Uviko 19 kabla ya kwenda kupiga tizi la maana na usiku wa leo timu imeenda Uwanja wa l’Amitie General Mathieu Kerekou utakaotumiwa kwa mchezo huo wa leo Jumapili utakaochezwa kuanzia saa 1:00 usiku.

Simba itawakosa Jimmson Mwanuke na Hassan Dilunga walio majeruhi

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger