Mrema Atangaza Kuoa Tena, Asema Amepata "Binti Mdogo"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwenyekiti wa TLP Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya PAROLE nchini Dk. Augustino Mrema ametangaza kufunga ndoa siku ya Alhamisi Machi 24,2022 katika Parokia ya Uwomboni kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Dk. Augustino Mrema.
Mrema anafunga ndoa hiyo mara baada ya kumpoteza mke wake Rose Mrema aliyefariki dunia Mwaka jana.

Mrema amesema amepata "binti mwenye umri mdogo" mweupe ambaye ni chaguo lake na watafunga pingu za maisha mara baada ya kufuata taratibu zote za kikanisa pamoja na ulipaji wa mahari .

Amesema kilicho msukuma kuoa ni kumpata msaidizi wa kumsaidia katika maisha yake kwani yeye ni mzee na anaitaji mtu wa karibu wa kumwangalia na kumsaidia kwa ukaribu.

Mrema amesema anashukuru familia yake kwa kumkubalia.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad