3/16/2022

Msuva Aitabiria Makubwa Simba CAF
MCHEZAJI wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye kikosi cha Raja Casablanca ya Morocco, Simon Msuva amesema kuwa kwa mwendo wa Simba wanaouonyesha kwenye michuano ya kimataifa watafika mbali.


Msuva kwa sasa anaripotiwa kuwa nchini hapa kwa madai yuko kwenye mgogoro wa kimaslahi na klabu yake hiyo ya Morocco.


Msuva ameliambia Championi Jumatano kuwa, Simba wameshakuwa wazoefu kwenye mashindano hayo na kubwa wamekuwa na uhakika wa kupata ushindi wakiwa nyumbani na angalau hata sare wakiwa ugenini jambo ambalo ni bora kwa mpira wa Afrika.“Simba nawaona wakifika mbali kwenye anga za kimataifa hasa kwenye mashindano haya ya kimataifa kwa sababu wana timu bora.


“Kwa mashindano ya Afrika ukiwa na uhakika wa kupata ushindi nyumbani na angalau sare ugenini, unakuwa na uhakika wa kufika mbali na Simba wanaweza kufanya hivyo.”

Simba wanashiriki Kombe la Shirikisho hatua ya makundi na ndio vinara wa kundi lao wakiwa na alama saba baada ya kucheza mechi nne.

STORI; ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger