MTU WA MPIRA: Nani alimsajili Fiston Mayele pale Yanga?KUNA Fiston Mayele mmoja tu mtu anayeifanya kazi ya kufunga kuwa rahisi kama vile kutafuna karanga. Mwanaume wa shoka kweli. Wakati anatua Yanga ilionekana kama ni mchezaji wa kawaida. Wengi walimbeza kutokana na rekodi zake za kawaida pale AS Vita ya DR Congo. Mayele hakuwahi kuwa tishio sana pale DR Congo.

Hata hivyo, tangu ametua Yanga amebadilika na kuwa mchezaji hatari. Anajua kufunga. Ana kasi na utulivu wa kutosha. Ni kiwango hiki cha Mayele kimetufanya tumuone Heritier Makambo kama mchezaji wa kawaida. Mayele anakupa kila kitu ambacho straika halisi anapaswa kutoa. Muda wote ananusa hatari.

Anakwenda na mikimbio ya timu. Anawapa viungo washambuliaji wigo mpana wa kumpasia mpira. Yupo imara kwenye mipira ya juu na chini. Ni mastraika wachache wenye uwezo huo.

Kwa sasa kwenye ligi yetu hakuna kazi ngumu kama kumkaba Mayele. Hata kama hatafunga, basi atawaacha mabeki wa timu pinzani wakiwa hoi.


 
Utakumbuka namna ambavyo Joash Onyango aliteseka kumkaba wakati wa pambano la watani mwishoni mwa mwaka jana. Onyango alilala hoi kwelikweli siku ile. Nadhani hatamani kukutana na Mayele katika siku za karibuni. Kama kuna lulu kubwa ambayo Yanga imejipatia katika eneo la ushambuliaji msimu huu ni nyota huyo kutoka DR Congo. Kwa bahati nzuri zaidi ni kombinesheni nzuri aliyotengeneza na Saido Ntibazonkiza siku za karibuni. Mayele anazitendea haki pasi za Saido. Anaifanya Yanga kuwa hatari katika eneo la mbele.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad