Ticker

6/recent/ticker-posts

MTU WA MPIRA: Viongozi Azam FC wajitathmini, timu imekwama

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>IPI timu tajiri zaidi nchini kuliko Azam FC? Hakuna. Si Simba wala Yanga, Azam ndio timu tajiri zaidi hapa Tanzania.

Kwanza inamilikiwa na familia ya bilionea Salim Said Bakhresa. Ni mtu mwenye fedha nyingi. Halafu mbali na hilo, familia hiyo inapenda sana soka.

Hii ndio sababu Azam hadi sasa ndio pekee inayomiliki uwanja wa kisasa. Ndio klabu yenye hosteli. Ndio timu inayomiliki mabasi ghali zaidi ya kubeba wachezaji. Yaani kwa kifupi ina kila kitu.

Fedha ambazo Mohamed ‘Mo’ Dewji amewekeza pale Simba ni za matumizi ya Azam kwa miaka minne au mitano tu. Sh20 bilioni ni fedha ndogo sana kwa Bakhresa. Ndio sababu nakwambia Azam ni timu tajiri.


 
Wakati Mo Dewji anatoa pesa kama hisani ama msaada katika matumizi mengine pale Simba, Bakhresa anatumia fedha kwa ajili tu ya furaha yake pale Chamazi. Hatoi msaada wala hisani ameamua kuwekeza katika soka. Ni kwa furaha ya Watanzania.

Pamoja na utajiri huu, bado Azam imekuwa timu ya kawaida sana katika ligi yetu. Ilianza kwa kasi katika miaka mitano hadi sita ya mwanzo, lakini sasa mambo yamekuwa tofauti.

Baada ya miaka michache Azam ilikuwa ikizitenganisha Simba na Yanga pale juu kwenye msimamo.


Baada ya miaka michache tu ikawa imetwaa taji la Ligi Kuu Bara. Ikatwaa mataji ya Mapinduzi na Kagame. Ilikuwa tishio kweli. Ni nyakati hizi mtendaji mkuu wa timu alikuwa Nassoro Idrissa ‘Father’. Kwenye benchi la ufundi walikuwepo watu wa soka. Alikuwa Jemedari Said kama meneja wa timu, wakawepo kina Philip Alando na wengineo. Watu wanaoufahamu vyema mpira wa Tanzania.

Chini ya utendaji wa Father, Azam iliishi katika uhalisia wa soka la Tanzania. Ilishindana na Simba na Yanga katika usajili. Ilichukua wachezaji Simba na Yanga. Iliweza kucheza mechi ngumu. Haikuonewa na waamuzi. Ilikuwa ikiishi sayari yake.

Hata hivyo, tangu Father ameachia kiti hicho watendaji wengine waliofuata wamefeli. Pengine zipo sababu za wao kufeli, lakini wengi wanaishi katika uongo uongo ambao unawapoteza na kuwakwamisha.

Mfano mzuri alikuja mtendaji mkuu anayeitwa Abdul Mohammed. Huyu akaamua kuachana na wachezaji wengi wakubwa klabuni hapo kwa madai kuwa wanalipwa fedha nyingi. Akaja na mpango wa kubana matumizi. Akawaondoa wachezaji wengine kwa madai kuwa wamechoka.

Akapunguza posho na gharama za fedha za usajili. Katika zama zake Azam ikaanguka kabisa. Ikapoteza ushindani iliokuwa nao katika ligi. Unakwendaje kubana matumizi kwenye timu ya tajiri? Ni kichekesho.

Uliwahi kusikia wapi watendaji wa Chelsea, PSG na Real Madrid wamekuja na mpango wa kubana matumizi? Moja ya sifa ya timu za matajiri ni kutumia fedha. Unakwenda sokoni unanunua wachezaji wakubwa na unawalipa vizuri. Lakini pale Chamazi mtendaji akaamua kubana matumizi. Baada ya anguko hilo, akaja mtendaji mkuu wa sasa, Abdulkarim Amin ‘Popat’. Nini kimebadilika? Hakuna!

Baada ya miaka minne ya Popat, Azam imeendelea kuwa ileile. Imeshinda taji moja la Kagame na FA. Mataji hayo walishinda katika misimu ambayo wakubwa hawakuwa na habari nayo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments