3/18/2022

Mwanamke Mtanzania Ampongeza Mumewe kwa Kumuolea Mke wa Pili, Pata Uhondo KamiliMkewe Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Azam FC aliiwasha mitandao baada ya kumkaribisha mke mwenza katika familia yake
Zainab Abdallah ambaye ni kamishna wa wilaya nchini humo alieleza kuwa yeye ndiye aliyemshauri mumewe kumuoa mwanamke mwengine
Zainab Abdalla, Mtanzania ambaye ni mkewe mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Azam FC Van Mohammed ameshangaza wengi baada ya kumpongeza mumewe kwa kumuoa mke wa pili kwani ni adimu kwa Mwanamke kumpongeza mumewe kwa kuongeza mke.

Mwanamke Mtanzania ampongeza mumewe kwa ya kumuoa mke wa 2, Uhondo kamili
Zainab Abdalla ambaye ni kamishna wa wilaya nchini Tanzania alimshukuru mumewe kwa kumuolea mke wa pili kufuatia harusi yao. Picha: Zainab Abdalla
Zainab Abdalla ambaye ni kamishna wa wilaya nchini Tanzania aliiwasha mitandao Jumatano Februari 21, 2018 baada ya kuchapisha picha ya mumewe na mkewe wa pili huku akimpongeza kwa hatua ya kumuoa mke huyo.

TUKO.co.ke imegundua kuwa Zainab amekuwa na shuguli nyingi za kazi na hivyo alimshauri mumewe kumuoa mke wa pili ambaye angesaidia katika majukumu ya nyumbani na kumhudumia mumewe.

“Nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi” aliandika Zainab kupitia ukurasa wake wa Instagram.


 

Read also
Kashfa ya NYS: Huenda Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru Akanaswa Kufuatia Kukamilika kwa Uchunguzi

Aluongeza, ”Namshukuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.”

Hatua hiyo iliyochukuliwa na Zainab iliwashangaza wengi, wakisalia kujiuliza ikiwa alikuwa na akili timamu.

Hata hivyo Zainab alieleza kuwa alichukua hatua hiyo akiashiria desturi za dini ya Uislamu.

Alidai kuwa Mungu amewabariki na pesa nyingi na hivyo haoni shida kula pamoja na wengine wasiojiweza.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger