Mwanamke Mwenye Kucha Ndefu Zaidi Duniani Hatimaye Azikata kwa Mara ya Kwanza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Ayanna Williams ambaye alishikilia rekodi ya 'Guinness World Record ya kuwa na kucha ndefu zaidi duniani, amezikata
Kulingana na Guinness, mshikilizi huyo wa zamani alishinda rekodi hiyo mwaka 2017 ambapo kucha zake zilikuwa zina futi 18
Alikuwa anatumia chupa mbili za rangi kurembesha kucha zake
Williams alivunja rekodi hiyo ya 2017 baada ya kucha zake kuwa na futi 24
Ayanna Williams, mwanamke anayeishi Texas ambaye alishikilia rekodi ya 'Guinness World Record ya kuwa na kucha ndefu zaidi duniani, hatimaye amezikata baada ya miaka 30.

Mwanamke Mwenye Kucha Ndefu Zaidi Duniani Azikata kwa Mara ya Kwanza
Mwanamke mwenye kucha ndefu zaidi duniani Ayanna Williams azikata kwa mara ya kwanza. Picha: Guinness World Records.
Lakini kulingana na Guinness World Record, alivunja rekodi yake ya kwanza baada ya kucha zake kuwa na futi 24 kabla ya kuzikata siku ya wikendi Aprili 7, 2021.

Williams aliweka rekodi hiyo mwaka 2017 ambapo kucha zake zilikuwa zina futi 18 na alikuwa anatumia chupa mbili za rangi kuzirembesha.

"Nimekuwa nikizifuga kucha zangu kwa miongo kadhaa sasa. Niko tayari kwa maisha mapya. Najua nitazikosa sana lakini wakati wa kuzitoa umefika."


 
Atletico Madrid Waondoa Man United kwenye Champions League
"Bado nitasalia malkia nikiwa nazo au la. Mimi ndio ninaunda kucha zangu ," alisema.

Aliambia Guinness namna alikuwa akimuomba mama yake kukagua urefu wa kucha zake kila mara.

Alikuwa anashindwa kufanya kazi za nyumbani ikiwemo kuosha vyombo na kutandika kitanda kwa sababu ya kucha zake ndefu


"Na shughuli zangu lazima niwe mwangalifu sana. Kwa hivyo kwenye akili yangu najaribu kuchukuwa tahadhari katika hatua yangu nyingine ili kuhakikisha sijiumizi na kucha zangu ama kuzivunja," Williams alisema.

Alisema anafurahia kukata kucha zake kwa sababu anatazamia kufungua kurasa mpya.

Williams alisema anaazimia kufuga kucha zake hadi inchi sita pekee.

Kulingana na Ripley, kucha zake alizokata zitawekwa katika makavazi mjini Orlando, Florida.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad