Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanasoka wa kwanza Afrika kuvunja mkataba Urusi

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>Mnigeria Sylvester Igboun (31) amekuwa Mwanasoka wa Kiafrika wa kwanza kuondoka kwenye Ligi ya Urusi kufuatia uvamizi uliofanywa na Urusi nchini Ukraine.

Igboun ametumia kanuni mpya ya FIFA inayowaruhusu raia wa kigeni wanaocheza mpira wa kulipwa nchini Urusi kusimamisha mikataba yao na kuondoka kwa muda.

Tofauti na ilivyotarajiwa, Mshambuliaji huyo ameamua kuuvunja mkataba wake na Klabu ya FA Nizhny Novgorod ambayo alijiunga nayo mwezi uliopita akitokea katika klabu ya Dynamo Moscow kwa makubaliano.

Igboun aliichezea klabu ya FC Midtjylland ya Denmark kabla ya kuhamia Urusi mnamo mwaka 2015.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments