3/07/2022

Nahreel wa Navykenzo Akanusha Habari za Kuwa na Mtoto wa Nje

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPAMsanii na Mtayarishaji maarufu wa muziki Bongo Emmanuel Mkono maarufu Nahreel amekanusha vikali taarifa za kuzaa nje ya mahusiano yake na mpenzi wake, Aika.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nahreel ametaka wote wanaosambaza taarifa hizo kuiheshimu familia yake na kusisitiza ana watoto wawili tu aliojaliwa na Aika.

"Kutokana na habari zinazosambaa kwenye blog mbalimbali na watu mbalimbali maarufu pia wamekuwa wakipost bila kuwa na ushahidi wowote, hizi habari sio za kweli.


Nina watoto wawili, Gold na Jamaika, na nimezaa na mwanamke mmoja Aika, kuweni makini mnapotoa habari familia yetu haiendekezi umbeya ila hii imevuka mipaka" - unasomeka ujumbe wa Nahreel.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger