Nandy Afumaniwa na Mwijaku, Akana Madai ya Kuchepuka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Mwanamuziki wa bongo fleva, Nandy amekanusha madai kwamba anachepuka baada ya mtangqazaji wa shirika la habari la Clouds kumfumania usiku akizindikizwa kwenye gari na mwanaume mwingine ambaye Mwijaku alibaini si yule ambaye amemchumbia juzi, Billnass.

Baada ya Mwijaku kumkuta akifunguliwa lango, alimzaba na maswali mazito ambapo Nandy alijikaza kujitetea kwamba yeye hachepuki na kusisitiza kwamba anajua ni mke wa mtu na pia kusema kwamba mumewe mtarajiwa anajua kwamba alikuwa sehemu hiyo katika harakati za kufanya video.


“Mwijaku mimi ni mke wa mtu, niko kwenye shooting na mume wangu anajua. Usinitafutie matatizo na nampigia simu sasa hivi adhibitishe,” Nandy anaonekana akijitetea.

Mwijaku alidadisi kwamba tqangu lini shooting ifanywe usiku kama huo wakati anagunguliwa lango na ikabidi amshrutishe Nandy kumpigia simu Billnass.

Billnass baadae alipokea simu na kudhibitisha kwamba alikuwa na habari ya kule ambako Nandy alikuwa na hapo angalau Mwijaku akakubali na kuwaacha waendelee na shughuli yao ya shooting.


“Nimemkuta sehemu Billnass, unajua kama yuko hapa sasa hivi? Unajua eh? Hapo sawa maanake nimeogopa nimekuta nyuma ina geti kali nyumba ina walinzi halafu nikaona kuna mwanaume alikuwa anamsindikiza ndio maana nikaogopa. Basi nashukuru, nimejiakiki kumbe kweli alikua anafanya kazi,” anasikika akisema Mwijaku.

Wiki jana Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba nyumbani kwao Nandy, Mlandizi na wawili hao wakafichua kwamba ndoa rasmi haitopita mwezi wa sita.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad