Nandy Alia na Upweke Kisa Billnass, Ndoa Kufanyika Kwenye Kifaru Cha Vita


NANDY au The African Princess ni malkia wa muziki Afrika Mashariki akitokea Tanzania ambaye ambaye amefunguka makubwa akilia upweke baada kuandika ujumbe kwenye ukurasa wa mchumba’ke, Billnass au Nenga akimtaka kurudi nyumbani haraka.

Billnass yupo Dubai ambapo inasemekana ameenda kwa shughuli za kibiashara.

Hivi karibuni Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba nyumbani kwao huku wakifichua kwamba ndoa rasmi haitapita mwezi wa sita.

Billnass alimjibu Nandy kwa kumueleza kuwa anatafuta vazi ambalo atavaa siku ya harusi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wao.


“Nandy nakutafutia gauni la harusi, maana hizi vita zinanichanganya, tunaweza kufungia ndoa kwa kifaru,” anasema Billnas akimaanisha vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Ni hivi majuzi Nandy amekanusha madai kwamba amechepuka baada ya mtangazaji wa shirika la habari nchini humo, kumfumania usiku akisindikizwa kwenye gari na mwanamume mwingine ambaye Mwijaku alibaini si yule ambaye amemchumbia juzi, Billnass

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad