3/07/2022

Netflix imesitisha Huduma zake Nchini Urusi Kupinga Urusi Kumvamia Ukraine


Netflix imesitisha huduma zake nchini Urusi ikiungana na orodha ya biashara za Magharibi zinazokata uhusiano na Urusi kupinga uvamizi wa Ukraine.

Huduma maarufu ya Netflix ilisema Jumapili kwamba inafunga kabisa huduma yake nchini Urusi "Kwa kuzingatia hali ilivyo, tumeamua kusitisha huduma yetu nchini Urusi"

Uamuzi wa Netflix unafuatia orodha ya kampuni za Magharibi zinazositisha shughuli nchini Urusi, Studio za filamu za Warner Brothers, Sony Pictures na Disney, kampuni mama ya ABC News, zimeondoa matoleo ya baadaye ya filamu nchini Urusi.

Ikea, Mastercard, Visa na American Express pia zimesitisha huduma kwa Urusi, Microsoft na Apple wamesitisha mauzo yote, ikijumuisha vifaa vya michezo na simu.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger