3/15/2022

Raia Walalamika Kutopewa AJIRA Mradi wa SGR

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Wananchi wa Fela Wilayani Misungwi wamesimamisha msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakilalamilia kunyimwa ajira katika mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka

Mwenyekiti wa Wananchi hao, Paulo Mrema amesema waliweka kambi eneo la mradi kwa muda mrefu wakisubiri kupatiwa Ajira, wengine wamelalamika kuombwa rushwa ili kupewa kazi

Aidha, inaelezwa kuwa Wananchi wengine hawakulipwa Fidia ya zaidi ya Tsh. Milioni 800 kwa maeneo ambayo yamechukuliwa kupitisha mradi huo. Mkuu wa Wilaya ya Misungwi amekiri Wananchi hao kutolipwa Fidia


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger