Rais Joe Biden amwita Putin kuwa mhalifu wa kivita

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wakatu hali ikiendelea kuwa mbaya nchini Ukraine, Rais Joe Biden wa Marekani amemwita rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa ni mhalifu wa kivita.


Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Kreamlin Dmitry Peskov amesema kitendo cha rais wa Marekani Joe Biden kumwita Rais wa Urusi kuwa mhalifu wa kivita hakikubaliki na hakisameheki. Habari hizo ni kwa mjibu wa shirika la habari la taifa hilo TASS.

Rais Joe Biden wa Marekani amemwita rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa ni mhalifu wa kivita, katika kipindi hiki ambacho matukio ya kikatili yakitajwa kuongezeka nchini Ukraine huku rais wa Ukraine akiliomba bunge la Marekani msaada zaidi.

Kauli hiyo inatazamwa kuwa kali zaidi kutoka Marekani tangu Urusi iivamie Ukraine. Wakati mataifa mengine yalitumia neno hilo lakini Marekani imekuwa ikijizuia.


 
Katika hotuba yake ya Jumatano Biden amesema vikosi vya Urusi vimeshambulia hosiptali na kuwachukua mateka madaktari. Hata hivyo ametoa ahadi zaidi kwa Ukraine katika kukabiliana kivita na Urusi. Amesema Marekani itatoa msaada wa nyongeza wa kijeshi wa kiasi cha dola milioni 800, na kufanya kiwango cha msaada kufikia jumla ya dola bilioni mbili tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.

Slovakia inatafakari kuipa Ukraine mfumo wa kujikinga na mashambulizi ya angani.


Maafisa wa ulinzi wa Slovakia wanatarajiwa kujadili uwezekano wa kupeleka mfumo wa ulinzi wa zama za uliokuwa umoja wa Kisovieti aina ya S-300 wa ulinzi wa anga, pale Waziri wa Ulinzi wa Marekani atakapo wasili nchini humo Alhamis hii kwa mashauriano zaidi.



Mfumo huo ndio ule ambao Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky aliutaja pale alipozungumza na wabunge wa Marekani kwa kusema utaweza kuifunga anga ya Ukraine dhidi ya mashambulizi ya anga ya Urusi na makombora yake.

.

Ndani nchini Ukraine, wizara ya mambo ya nje imesema vikosi vya Urusi vimelishambalia jengo la micherzo la mji wa mji wa Mariupol, ambalo inadaiwa mamia ya watu wamepatiwa hifadhi baada ya makazi yao kuharibiwa na mapigano. Shambulizi kutoka angali linaelezwa kulipasua katikati jengo hilo.


 
Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko amesema makombora ya Urusi yameharibu maeneo kadhaa ya makazi ya watu na hasa katika kitongoji cha Podii, umbali wa kilometa 2.5 kutoka katika makao makuu ya serikali, ambayo pia yanajumuisha makazi ya rais, ofisi ya rais na ofisi nyingine muhimu.

Lakini taarifa hiyo haikuweza kufafanua juu ya athari zaidi zilizotokea kama kuna vifo au la. Wakazi wa Kyiv wamejificha katika makazi yao na maeneo maalumu baada ya kutolewa marufuku ya kutoka nje. Habari za mapema mjini humo zinasema jengo la ghorofa 12 liliwaka moto baada ya kushambuliwa na makombora ya Urusi.



Huko mjini Melitopol, Meya wa mji huo wa kusini/mashariki ameachiwa huru baada ya kutekwa na majeshi ya Urusisiku tano zilizopita. Andriy Yermak mkuu wa majeshi wa taifa hilo alitoa taarifa hizo pasipo ufafanuzi zaidi wa namna gani Fedorov aliachiwa huru.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad