3/16/2022

Rais Samia Awagusa WanaojichubuaRais Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania wa hali yoyote nchini kujikubari na hali ya maumbile yao na sio kujikata kwa kufanya mambo mbalimbali kujibadilisha.

Akizungumza kwenye hafla maalum na watu wenye ulemavu iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma Rais Samia amesema kasumba hiyo haipo kwa watu wenye ulemavu pekee bali hata kwa watu wenginew huku akitolea mfano wanaojichubua.


"Na tatizo hili sio lenu peke yenu, hata wale ambao wanaonekana kwamba ni wazima, wengi hatujikubali tulivyo, aliye mweusi atajichubua awe mweupe hajikubali alivyo,  mwenye nywele za kiafrika ataenda kutia za kizungu hajikubali alivyo kwa hiyo ni tatizo" amesema Rais Samia.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger