3/17/2022Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema leo kuwa operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imefanikiwa na kuwa hatoiruhusu nchi hiyo kutumika kama uwanja wa kuitishia Urusi. 

Akizungumza katika mkutano wa serikali uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni, Putin amesema operesheni yake inaendelea vizuri kwa kufuata kikamilifu mipango waliyoiweka. 

Rais huyo ameongeza kuwa benki kuu ya Urusi haina haja ya kuchapisha pesa kwa kuwa nchi hiyo ina rasilimali za kutosha za kifedha za kukabiliana na changamoto za sasa za vikwazo. 

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili za kivita yanaendelea kwa sasa huku kila mmoja akielezea matumaini ya kupatikana suluhu

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger