Saido kuikosa KMC...Avuta jik 
Saido aliye majeruhi hatakuwa sehemu ya mchezo wa Jumamosi hii kati ya timu yake Yanga na KMC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
NYOTA wa Yanga, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ anatarajia kufunga ndoa Jumamosi, Machi 19 na mpenzi wake Uwera Samantha ‘Samira’.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari  na mitandao ya kijamii nchini Burundi ndoa hiyo itafanyika kwa taratibu za dini ya kiislamu na baadae sherehe zitaendelea kwenye ukumbi wa Beliane, Bujumbura.

Saido aliye majeruhi hatakuwa sehemu ya mchezo wa Jumamosi hii kati ya timu yake Yanga na KMC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kadi ya mwaliko wa harusi ya Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ anatarajia kufunga ndoa Jumamosi, Machi 19 na mpenzi wake Uwera Samantha ‘Samira’.

Tayari nyota huyo yupo kwao nchini Burundi akikamilisha taratibu za ndoa hiyo na atatumia kipindi cha Ligi kusimama zikipisha ratiba za timu za taifa kama fungate kabla ta kurejea Tanzania kujiunga na Yanga.

Nyota huyo amekuwa na kiwango bora msimu huu ndani ya Yanga akihusika kwenye mabao 10 ya chama hilo kwenye Ligi kwa kufunga matano na kutoa asisti nne.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad