3/16/2022

Tofauti ya Wasanii wa Tanzania na wa Nigeria


Kwanza kabisa tukubali jamaa wa west africa wako mbali sio wasanii peke yao hata vijana wa kule ni tofauti na sisi wa huku Tanzania anzia mawazo hadi vision ya maisha. Na yafuatayo ni yale mapoint yanayotofautisha wasanii wa Tanzania na Nigeria


🍁Tanzania wasanii wengi ni Maskini na fukara Nigeria wengi wao wanajiweza kipesa na matajiri.

🍁Wasanii wa Tanzania wengi wanaishi maisha ya kujidanganya wao wenyewe na kujipa thamani wasiyokua nayo wakati Nigeria wasanii hawafanyi hivo.

🍁Tanzania wasanii hawana umoja kabisa na wanaishi kinafiki wakati Nigeria wasanii wana umoja mkubwa sana hata pakitokea sintofahamu wanaimaliza mapema iwezekanavo.

🍁Wasanii wa Tanzania hawapati kile wanachostahiki kutokana na jasho lao wakati wanaigeria kuanzia mauzo na stahiki zao kwenye kazi zao za sanaa zinawabeba sana.

🍁kazi za wasanii wa Kitanzania hazifiki kwenye masoko yenye pesa duniani kwa maana Amerika na ulaya Wakati wenzao wa Nigeria kazi zao zinapenya kwenye masoko ya maana.

🍁wasanii wa Tanzania wengi hutumika kwenye majukwaa ya kisiasa kwa malipo kidogo wakipewa na kofia ndio imetoka Wakati wasanii wa Nigeria hutowaona hovyo kwenye majukwaa ya kisiasa.

🍁Wasanii wa Tanzania hawana miradi endelevu ya kiuchumi Wakati Nigeria wanajali uwekezaji endelevu kwa mfano psquare hawana njaa hadi leo wakati Juma nature wetu hali sio hali na analilia collabo na madogo.

🍁Wasanii wa Tanzania wanapenda kupanga majumba ya kifahari ya watu wengine Wakati Wasanii wa Nigeria wanapenda kujenga majumba yao ya kifahari.

🍁wasanii wa Tanzania hawapendi kujenga vijijini kwao Wakati wasanii wa Nigeria wanapenda kujenga vijijini kwao.

🍁Wasanii wa Tanzania wengi wao shule hamna kabisa wakati Wasanii wa Nigeria wengi Wao ni Wasomi wa fani mbali mbali. Mfano Niara Marley na 2face ni watu wenye Masters Degree kabisa na sio za mchongo!!

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger