3/07/2022

Ukatili; Raia Wanaokimbia Vita Wapigwa Mabomu Ukraine

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza HAPATuhuma kuhusu majeshi ya Urusi kuwashambulia raia wa Ukraine zinazidi kuongezeka ambapo katika matukio ya hapo jana, raia wanaokadiriwa kufikia nane wameuawa wakati wakijaribu kukimbia mapigano katika Mji wa Irpin na wengine kadhaa wakiuawa katika Mji wa Mauripol.

Picha na video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zinawaonesha maelfu wa wakazi wa Mji wa Irpin ulioshambuliwa vikali na majeshi ya Urusi hapo jana, wakitafuta njia za kutorokea kukimbia mashambulizi ya makombora ya Marekani huku jitihada za kuwaokoa maelfu ta raia walionasa katika Mji wa Mauripol, zikikwama kwa mara ya pili.

Habari mbaya ni kwamba, miongoni mwa wanaojaribu kutoroka, siyo wote wanaofanikiwa kutoka salama kwenye miji hiyo miwili ambayo mpaka usiku wa kuamka leo, ilikuwa ikiendelea kushambuliwa vikali na majeshi ya Urusi.

Picha za wananchi wengi wakiwa wameuawa baada ya kupigwa makombora, zinaendelea kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuzigusa hisia za wengi.

Kinachozidi kusikitisha zaidi ni kwamba miongoni mwa wanaouawa, wapo wanawake na watoto ambapo Waziri wa Nchi wa Marekani, Anthony Blinken ameonya kwamba kinachofanywa na Urusi nchini Ukraine, ni uhalifu wa kivita ambao hauwezi kufumbiwa macho.


 
Miongoni mwa picha zilizogusa hisia za wengi, ni ile inayomuonesha mwanaume akiwa amembeba mwanaye kwenye umri wa miezi 18 akimkimbiza hospitali, baada ya familia yake kushambuliwa na makombora ya Urusi.

Licha ya jitihada za kumkimbiza mtoto huyo hospitali, alifariki dunia ambapo katika picha nyingine, mwanaume huyo anaonekana akilia kwa uchungu kando ya mwili wa mwanaye akiwa na mkewe.

Katika picha nyingine, miili ya mwanamke mmoja na wanaye, inaonekana ikiwa imelala kando ya barabara na kuzungukwa na mabegi, hali inayoonesha kwamba familia hiyo ilikuwa ikijaribu kutoroka kutoka katika Mji wa Irpin.


Ukiachilia mbali Mji wa Irpin ambao umechakazwa vibaya na makombora ya Urusi na kusababisha maafa makubwa, mji mwingine wenye hali mbaya ni Mauripol.

Jitihada za kuwatoa wananchi katika mji huo zimakwamishwa kwa mara nyingine baada ya majeshi ya Urusi kuendelea na mashambulizi hapo jana licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano ili kupisha raia kuondolewa kufikiwa.

Hii ni mara ya pili kwa zoezi la kutengeneza njia salama (safe corridor) kwa ajili ya kuwaondoa raia waliokwama katika Mji wa Mauripol kushindikana, mara zote sababu ikiwa ni Urusi kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano katika baadhi ya maeneo ili kuruhusu raia waondolewe.

Wakati hayo yakiendelea, mke wa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine, Olena Zelenska amevitaka vyombo vya habari vya kimataifa, kueleza hali halisi ya kinachofanywa na majeshi ya Rais Putin nchini Ukraine, kwamba wanawake na watoto wanauawa.


 
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Olena Zelenska amesema tangu Ukraine ilipovamiwa na majeshi ya Urusi Februari 24, watoto wengi wamepoteza maisha na kuutaka Umoja wa Kujihami wa Nato, kulifunga anga la Ukraine ili kuzuia mashambulizi ya angani kutoka kwa majeshi ya Urusi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger